Balozi wa China nchini Tanzania Dr.Lu Youqing (katikati) akipata maelekezo kuhusu bidhaa za Huawei wakati wa mkutano wa watanzania waishio uhaibuni (Tanzania Diaspora).Kushoto ni Afisa mahusianao na habari,Jimmy na kulia ni Meneja wa bidhaa na huduma wa Huawei hapa nchini, Joseph Lyimo Huawei walikua ni wazamini wakuu wa mkutano huo ulifanyika jijini Dar es salaam katika hoteli ya Serena  Augost 14 mwaka huu.

  Dr.Lu Youqing lieleza kuwa sasa hivi China na Tanzania wana ushirikiano mzuri ambapo China imekuwa ikisaidia ukuaji wa uchumi wa Tanzania kwa kuwawezesha watanzania waliopo nchini China.

 Mbali na hayo wamekuwa wakisaidia Tanzania kwa njia nyingi moja wapo kwa makampuni ya nchi yao kuwekeza nchini Tanzania.

 Huawei ni moja ya kampuni hizo ambapo ina wafanyakazi wengi watanzania na imekuwa ikisaidia watanzania katika mambo mengi ya kielimu na kiteknolojia na kupelekea kukuza uchumi wa tanzania.
  Balozi wa China nchini Tanzania Dr.Lu Youqing akiwa kakatika picha ya pamoja na mameneja wa Huawei,wa kwanza kutoka  kushoto ni Jane Wang Jin afisa masoko wa Huawei na wa pili kutoka kushoto ni Mr.Jimmy Afisa mahusiana na mawasiliano akifuatiwa na mama Mulamula. Wengine ni wafanyakazi wa Huawei Tanzania. Hii ilikua katika mkutano wa watanzania waishio ughaibuni (Diaspora).
 Huawei Tanzania walikua moja ya wadhamini wa kongamano hili la siku mbili ambapo kampuni ya Huawei walionyesha jinsi Kamera za CCTV zinavyofanya kazi katika lango kuu la kuingilia katika kongamano  hilo ambapo kamera hizo zilionyesha vyema jinsi ya kumwona mtu ambaye anaweza kufanya uharifu wowote mahali pale.
Pia Huawei walikuwa na redio za 4G ambazo walikuwa wakizionyesha katika mabanda kabla na baada ya wanatanzania waishio ughaibuni kuingia na kutoka kujionea vifaa hivyo vinavyofanya kazi.
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete,akiwapongeza kampuni ya Huawei kwa kuwapatia cheti cha kudhamini kongamano la watanzania waishio ughaibuni ambapo kampuni ya huawei iliwakilishwa na Meneja wa Huawei hapa nchini, Jimy Jinglio.
 China imekua na ushirikiano mzuri na Tanzania na imetoa kipaumbele kwakufadhili kongamano la wanaDiaspora nje ya nchi kwa kuwapatia elimu na vitu vingine. 
Mbali na Hapo China imewekeza mambo mbalimbali nchini Tanzania hasa katika Elimu na Teknologia.
Waziri wa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa,Bernad Membe akipewa maelekezo na Mhandisi wa teknologia wa kampuni ya Huawei hapa nchini,Lameck Mangu mara baada ya kutembelea banda la maonyesho la HUWAWEI. HUWAWEI wakiwa na moja ya kampuni zilizodhamini mkutano uliowakutanisha watanzania waishio ughaibuni (Diaspora) katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Waziri wa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa,Bernad Membe amwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete kufungua mkutano uliowakutanisha watanzania waishio ughaibuni uliofanyika  katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...