Na Teresia Mhagama

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage amefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini Awamu ya Pili inayotekelezwa pembeni ya bomba kubwa la gesi katika mkoa wa Mtwara.

Pamoja na kukagua miradi hiyo inayofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na kutekelezwa na shirika la Umeme nchini (TANESCO), Naibu Waziri pia amekagua maendeleo ya kituo cha kuchakata gesi kilichopo kijiji cha Madimba katika mkoa wa Mtwara.

Katika ziara hiyo Mwijage ameagiza kuwa vifaa vya umeme vinavyohitajika katika utekelezaji wa miradi hiyo ya umeme, viwasilishwe ndani ya wakati uliopangwa ili miradi hiyo itekelezwe kwa ufanisi.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage ( mwenye suti ya bluu, kulia) akiangalia zoezi la uwekaji nguzo za umeme katika kijiji cha Sinde B, mkoani MTWARA wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (mwenye suti ya bluu ) akisalimiana na wafanyakazi wa kampuni ya Kusambaza Gesi (GASCO) walioko katika kituo cha kuchakata gesi cha Madimba mkoani Mtwara mara alipowasili kituoni hapo kukagua mitambo ya kuchakata gesi.Kushoto kwake ni Kaimu Meneja wa Kampuni ya Kusambaza Gesi (GASCO), Kapuulya Musomba .
Baadhi ya mitambo ya kuchakata gesi katika kituo cha Madimba mkoani Mtwara. Gesi asilia itasafishwa katika kituo hicho kabla ya kusafirisha kwa bomba la Gesi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...