
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Mwenza
wake, Dkt. Juma Haji Duni wakiwapingua maelfu ya wafuasi wa vyama vya
Siasa vinavyounda UKAWA, jijini Dar es salaam, Augusti 10, 2015,
walipokuwa wakielekea Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuchukua Fomu ya kuwania
Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba
25, mwaka huu.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akipokea fomu za tume ya Taifa ya Uchaguzi kkugombea nafasi hiyo, kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akisalimiana
na Mkurugenzi wa tume ya Taifa ya Uchaguzi, Kailima Ramadhan Kombwey,
baada ya kukabidhiwa fomu za tume hiyo za kugombea kiti cha Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Agosti 10, 2015. Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama cha
Wananchi CUF na Mgombea Urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif.
KUONA PICHA ZAIDI
I am speechless..............
ReplyDeleteNi kama mwaka 1995 kwa mchungaji mtikila na Mrema kwa wachambuzi wa mambo wanasema watamshangilia lakini hawatamchagua na kiashilio ni kukosekana kwa wanawake
ReplyDeleteKwa mtazamo huu naona ni kheri Dr. Slaa akaja kumuunga mkono EL kwenda ikuluitamletea heshima kubwa sana. kuliko kuendelea kujishimbia nyumbani.
ReplyDelete"Kiashirio kukosekana kwa wanawake",pengine una point hapo mdau. Kwani wakirudi makwao anapewa ultimatum, hupati chakula cha usiku kama utaendelea shabikia chama kingine, njemba taratibu anajirudi, no offence intended.On a serious note nakubaliana na mdau, kwani mashibiki wote ni wanaume, wanawake wapo wapi? pengine ni testosterone surge tu hiyo lakini mioyo yao pengine bado ipo CCM.
ReplyDelete