Afisa uhusiano mwandamizi Bw. Fulgence Sebera akitoa maelezo ya shughuli za Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) kwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Majid Mwanga (wa tatu kulia) aliyeambatana na viongozi wengine wa TASO walipotembelea banda la SSRA katika sherehe za maonesho ya wakulima Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere mkoani Morogoro.
Mch. Vernon Fernandes (aliyekaa) alipotembelea banda la SSRA katika maonesho ya Nanenane Morogoro, kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji Bi Sarah Kibonde Msika akifuatiwa na mwanasheria mwandamizi Bw. Omar Sururu Khalfan, kushoto ni Afisa matekelezo Bw. David Lyanga.
Mkuu wa kitengo cha uhusiano na uhamasishaji Bi Sarah Kibonde Msika wa kwanza kushoto akitoa maelezo ya masuala ya Hifadhi ya Jamii kwa wadau waliotembelea banda la SSRA, akifuatiwa na afisa matekelezo Bw.David Lyanga na afisa uhusiano mwandamizi Bw. Fulgence Sebera katika maonesho ya Nanenane Morogoro.
Maafisa wa Mamlaka wakikabidhi zawadi ya Mfuko wa SSRA kwa mdau aliyetembelea banda la Mamlaka katika maonesho ya Nanenane mkoani Morogoro.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...