Waziri mkuu mstaafu Edward
Lowassa ambaye ni mgombea Urais kupitia chama cha demokrasia na
maendeleo (CHADEMA)anatarajiwa kupokelewa kwa mapokezi makubwa ikiwemo
magari,pikipiki,katika uwanja wa ndege wa kia hadi viwanja vya
tindigani kata ya kimandolu jijini Arusha siku ya jumamosi(kesho tarehe
15) ambapo atahutubia wananchi katika mkutano ulioandaliwa na chama
hicho
Akizungumza mapema jana na
waandishi wa habari katika ofisi za chama hicho juu ya maandalizi hayo
Mwenyekiti wa chadema Mkoa wa Arusha Amani Golugwa alisema kuwa mapokezi
hayo yamekamilika kwa asilimia miamoja na tukiohilo ni la kihistoria
Alisema kuwa lengo
la ujio huo ni kumtambulisha mgombea urais ambaye ataambatana na mgombea
mwenza Juma Duni Hajji ,kwa kuwatambulisha kwa wananchi wa Mkoa wa
Arusha sambamba na kupata udhamini wa wananchama waliojiandikisha kupiga
kura
Pia alisema kuwa zoezi la
udhamini umeshaanza Arusha na uongozi wa Tume umaelekeza mgombea kupata
wadhamini 300 na jimbo la Moshi mjini wataoa wadhamini 300
Aidha aliwataka ,wakazi wa
jijili la Arusha na waliopo jirani kujitokeza kwa wingi katika tukiohilo
la kihistoria ambapo pia viongozi wakuu wa chama hicho watahudhuria
akiwemo Mwenyekiti wa Taifa Freeman Mbowe,wenyeviti wenza wa ukawa
kutoka NLD,NCCR pamoja na chama cha CUF,John Mnyika ,Nibu katibu
mkuuZanzibar Salum Mwalimu na viongozi wengine wengi
“Kwakushirikiana na jeshi la
polisi pamoja na vikosi vyetu suala la Amani,Utulivu,Ulinzi na Usalama
vitadumishwa katika msafara huo pamoja na mkutano huo”Alisema Golugwa
Hata hivyo baada ya mkutano huo
kuisha msafara huo utaelekea katika jimbo la Monduli ambapo pia
Mh.Lowassa atapata wasaa wa kuhutubia wananchi katika jimbo hilo
Kwa upande wake Naibu katibu
mkuu waTimu Lowassa for president Ndama Jeuri alisema wamejiandaa
vizuri kumpokea na wataendelea kuhamasisha watu kumuunga mkono Lowassa
katika harakati zake za Urais
Katika msafara huo
zaidi ya magari 75 yataanzia katika ofisi za chadema hadi katika uwanja
wa ndege wa kia huku vikundi mbalimbali vya ngoma vikitumbuiza wakati wa
mapokezi ya Lowassa.
Mwenyekiti wa chadema Mkoa wa Arusha Amani Golugwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya mapokezi ya mgombea Urais Edward Lowassa kupitia CHADEMA yamekamilika kwa asilimia miamoja na tukio hilo kuliita la kiistoria ambalo litafanyika katika viwanja vya tindigani kata ya kimandolu jijini Arusha siku ya jumamosi(kesho tarehe 15)(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha kupitia chama cha CUF Salussingo Omari akizungumza na vyombo vya habari.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...