Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Fatma Salum Ally akifungua mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana kupitia
mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, yaliyofanyika kwenye Ukumbi VETA mjini
Mtwara jana.
Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi akizungumza wakati
wa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’,
yaliyofanyika kwenye Ukumbi VETA mjini Mtwara jana.
Meneja wa Airtel Mtwara, Bartholomew Masatu akitoa mada kuhusu fursa
mbalimbali zinazoweza kuwakwamua vijana kiuchumi, wakati wa mafunzo ya
ujasiriamali kwa vijana kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, yaliyofanyika
kwenye Ukumbi VETA mjini Mtwara jana.
Mkufunzi kutoka Mpango wa Anzisha na Boresha Biashara yako (SIYB)
ulio chini Shirika la Kazi Duniani (ILO), Fidelis Madaha akitoa mada wakati wa
mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’,
yaliyofanyika kwenye Ukumbi VETA mjini Mtwara jana.
Mkuu wa Wilaya ya
Mtwara, Fatma Salum Ally (kulia), akijadiliana jambo na vijana walionufaika na
fursa za Airtel (kutoka kushoto), Iddy Salum Chilumba, Godfrey Frank Manjavila
na Prisca George Chilumba baada ya kufungua mafunzo ya ujasiriamali kwa
vijana kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, yaliyofanyika kwenye
Ukumbi VETA mjini Mtwara jana. Wanaoshuhudia ni Meneja wa Huduma kwa Jamii wa
Airtel, Hawa Bayumi (wa pili kulia) na Meneja wa Airtel Mtwara, Bartholomew
Masatu.
Vijana mkoani Mtwara
wametakiwa kutumia fursa za uwepo wa nishati ya mafuta na gesi katika kukuza
biashara zao na uchumi wa mkoa huo.
Wakizungumza mara baada ya
kumalizika kwa mafunzo ya ujasiriamali mkoani humo, baadhi ya vijana hao
wamesema kuwa fursa zilzizopo mkoani humo ni lazima ziwanufaishe vijana ili
waendane na ukuaji wa uchumi wa mkoa huo.
Kampuni ya Airtel Tanzania, kupitia mradi wake wa “Airtel Fursa Tunakuwezesha” imewapatia mafunzo na kuwawezesha mitaji baadhi ya vijana wa manispaa ya mtwara kwa lengo la kuwawezesha kumudu uendeshaji biashara zao na kukuza mitaji yao.
Idd Abdallah ni
mjasiriamali aliyenufaika na mafunzo hayo ambaye anasema kuwa kwa sasa amepata
muongozo mzuri utakaokuza biashara zake na kuzifanya kwa weledi mkubwa zaidi.“Hii ni fursa ya kipekee
kwangu kama kijana na ninaishukuru sana Airtel kwa mafunzo yenye manufaa kwangu
na vijana wenzangu wa hapa mtwara” Alisema Abdallah.
Nae mkuu wa wilaya ya Mtwara bi.Fatuma Ally, alisema “mafunzo haya yatapanua wigo wa ufahamu kwa vijana hawa ambapo aliwataka kujituma kwani fursa zipo nyingi mkoani humo.
“Mtwara kuna maeneo mengi
sana yenye fursa kwa vijana kujiendeleza hivyo nawataka vijana kutumia fursa na
mafunzo haya kuhakikisha wanajiendeleza kiuchumi” alisema mkuu huyo wa wilaya.
Hawa Bayumi ni Meneja Maendeleo
ya Jamii wa Airtel, alisema hiyo ni fursa inatolewa na Airtel kwa lengo la
kusaidia vijana kupata fursa ya kujiajiri na kupata mitaji kupitia mpango huo.
“Kwetu sisi Airtel tunaona
ni fahari kuwawezesha wajasiriamali kwa mafunzo na mitaji ili waweze kuendeleza
biashara zao na kukuza mitaji pia. Alisema Bayumi.
Ugunduzi wa gesi na mafuta mkoani hapa, vijana wanapaswa kujituma kwa kuongeza elimu na mitaji ili waweze kuwa sehemu ya wanufaika na kuondoka na hali ya kuwa watazamani wa tunu hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...