Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Aziz Ponary Mlima aliwaalika Mabalozi wa wa nchi mbali mbali kuja kutembelea Tanzania hivi karibuni.
Mabalozi hao kutoka Kuala Lumpur Malaysia walitembelea mbuga za wanayama za Serengeti, Ngorongoro na walifanya ziara mjini Zanzibar.
Mabalozi hao ni Waheshimiwa Viorica na Constantin Nistor (Romania), Stephen Mubiru (Uganda), Dkt. AzizPonary Mlima(Tanzania), Isabela Mhlanga( Afrika Kusini), na Bwana Rogatius Shao (Naibu Balozi-Tanzania).
Mabalozi walipowasili Kibo Palace Hotel, Arusha na kupokelewa na Naibu Waziri wa Maliasili.na Utalii Mheshimiwa Mahmud Mgimwa, Bwana Alan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA na Bwana Pascal Shelutete Meneja wa Mawasiliano na Masoko wa TANAPA.
 
 Tembo mbugani Serengeti
 Simba wa Serengeti
 Kifaru katika mbuga ya Serengeti
 Mabalozi walipowasili kutokea Zanzibar
Mabalozi hao walikutana na  Balozi Thami Mseleku ambaye ni Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania na Balozi Chabaka Kilumanga na Mkewe katika  Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam kabla ya kuondoka na kurejea Kuala Lumpur.
Sehemu ya mamilioni ya nyumbu na pundamilia Serengeti

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...