Hatimaye mafunzo ya huduma ya leseni kwa njia ya mtandao kwa wachimbaji madini mkoani Kigoma yamemalizika. Mafunzo hayo yamehudhuriwa na wachimbaji madini zaidi ya mia moja.

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo, Afisa Madini Mkazi- Kigoma, Adam Juma aliwataka wachimbaji madini mkoani humo kuhakikisha wanafika Ofisi za Madini-Kigoma kwa ajili ya kusajiliwa kwenye mfumo huo.

Alisema ni vyema wachimbaji hao wakafanya hivyo mapema ili waanze kutumia mfumo huo ili kwenda sambamba na kasi ya ukuaji wa tekonolojia duniani.
Afisa Madini Mkazi- Kigoma, Adam Juma akifungua mafunzo hayo ya Huduma za Leseni kwa Njia ya Mtandao kwa wachimbaji madini wa Mkoani Kigoma (hawapo pichani). Kushoto kwake ni wataalamu kutoka Wizarani-Kitengo cha Leseni Idd Mganga akifuatiwa na Mhandisi Edward Mumba. Kulia kwake ni Viongozi wa Chama cha Wachimbaji Wadogo Kigoma (KIGOREMA), Karoli Ndimaso na Augustino Ruronona.
Baadhi ya wachimbaji madini Mkoani kigoma waliohudhuria mafunzo hayo wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo ambayo yamelenga kuwajengea uwezo wa kuelewa namna ambavyo mfumo huo unavyofanya kazi.
Baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini Mkoani Kigoma wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini wakati wa Mafunzo ya Huduma za Leseni kwa Njia ya Mtandao (OMCTP) yaliyofanyikia Mkoani humo na kuhudhuriwa na wachimbaji madini zaidi ya mia moja kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...