Mgombea Ubunge wa Jimbo la Dodoma,Antony Mavunde akionesha fomu alizochukua za kugombea Ubunge katika jimbo hilo nje ya ofisi za Halmashauri ya Dodoma. 
 Mgombea wa nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Dodoma Mjini,Antony Mavunde akipungia mamia ya mashabiki wakati akielekea katika ofisi za Mkurugenzi wa Halmashauri ya Dodoma kwekuchukua fomu.
 Mavunde akifurahia jambo na Wafuasi wake.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Dodoma Mjini kupitia chama cha Mapinduzi,Antony Mavunde akikabidhiwa fomu na Afisa Uchaguzi wa Jimbo la Dodoma Elizabeth Gumbo jana Mjini Dodoma.
MGOMBEA wa nafasi ya ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Anthony Mavunde amechukua fomu na kuahidi kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha analinda haki za wakazi wa mji wa Dodoma katika masuala ya ardhi.
 
Akizungumza na wanachi mara baada ya kuchukua fomu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) Mavunde amesema akipata nafasi ya kuwa mbunge kupitia nafasi hiyo atakuwa mjumbe wa bodi ya Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu(CDA),hivyo atahakikisha mamlaka hiyo inaboresha maisha ya watu na sio kuyadidimiza.

Aidha ameahidi kuimarisha sekta ya michezo ambayo imepewa kisogo katika Mkoa wa Dodoma.Michezo hiyo ni Pamoja na Mpira wa pete,Kikapu,Mpira wa mikono na Riadha,Mavunde alisema kama akipewa ridhaa ya kuwa Mbunge wa Dodoma basi suala la michezo kwake litakuwa ni la lazima na inapiga hatua.

"Mimi ni muumini wa michezo hivyo tofauti na soka nitatoa nafasi pia kwa michezo mingine ambayo imekuwa ikiipa sifa mkoa wa Dodoma ili vijana waweze kujikwamua na kuondokana na tatizo la ajira, "alisema

Alisema akipata nafasi ya kuwa Mbunge wa Dodoma basi cha kwanza atakachofanya ni kukutana na viongozi wote wa vyama vya michezo mkoani hapa ili kuweka kalenda za kisasa ambazo zitaendeleza michezo.

Mavunde alisema lengo lake lingine ni kuanzisha academic ya michezo ambayo itakuwa ikiwaandaa vijana jinsi ya kuwa wachezaji wa kulipwa katika miaka ya baadae pamoja na kuwatafutia soko la kwenda kuonyesha vipaji vyao nje ya Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. NAONA MHESHIMIWA ANASINDIKIZWA NA WATU WALIOVAA MIWANI NA KUASHIRIA KAMA VILE WAO NI WANAJESHI. HII NI BORA IPELEKWE RIPOTI KWA KAMANDA WA POLISI WA MKOA NA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI. HAIWEZEKANI WATU WAVAE MIWANI NA KUWA KAMA MA BODY GUARD, HII INATISHA WANANCHI NA INAHATARISHA AMANI. HII INAWEZA KUWA KAMA MAJESHI BINAFSI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...