Hatimaye mafunzo ya matumizi ya mfumo wa huduma ya leseni kwa njia ya mtandao yaani Online Mining Cadastre Transactional Portal (OMCTP) kwa wachimbaji madini mkoani Katavi yamemalizika.
Mafunzo hayo ya siku moja yamefanyikia kwenye ukumbi wa mikutano wa Idara ya Maji, mjini Mpanda na kuhudhuriwa na wachimbaji wadogo wa madini kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa huo yakiwa yamelenga kuwapatia uwezo wachimbaji madini wa kuutumia mfumo huo.
Akizungumza kwa niaba ya Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda Magharibi-Mpanda, Mhandisi Gilliard Luyoka aliwakumbusha wachimbaji hao kuhakikisha wanafika kwenye Ofisi ya madini ili kusajiliwa kwa ajili ya kutumia mfumo huo.
Pamoja na malengo mengine, inaelezwa kwamba Mfumo huo umeanzishwa ili kutekeleza agizo la Serikali la kutaka Wizara na taasisi za Serikali ziwe zinapokea malipo ya Serikali kwa njia za kielektroniki.
Mfumo wa Huduma za Leseni kwa njia ya mtandao ulizinduliwa rasmi mnamo tarehe 8 Juni, 2015.
Mhandisi
Gilliard Luyoka akizungumza kwa niaba ya Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda
Magharibi-Mpanda wakati wa mafunzo hayo
Mtaalamu
kutoka Wizara ya Nishati na Madini Kitengo cha Leseni, Idd Mganga akiwasilisha
mada wakati wa mafunzo hayo.
Baadhi
ya wachimbaji wadogo wa madini wakifuatilia mafunzo hayo
Mwenyekiti
wa KATAREMA, William Mbogo (kulia) akiuliza swali kwa Mtaalamu kutoka Wizara ya
Nishati na Madini, Idd Mganga (kushoto)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...