Umati wa Wakazi wa mji wa Tengeru, ukiwa umefurika kwa wingi barabarani kumlaki Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Edward Lowassa alipopita eneo hilo, wakati akielekea Jijini Arusha kwenye Mkutano wa hadhara wa kutambulishwa kwa Mgombea huyo kwa wananchi wa Arusha,uliofanyika kwenye Uwanja wa Kamandolu, leo Agosti 15, 2015.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Edward Lowassa na Mgombea Mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni wakiwa wamesimama pamoja na wananchi wa Jiji la Arusha walifurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Kamandolu, leo Agosti 15, 2015, wakati wa kuimba wimbo wa Taifa.
Muasisi Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mzee Edwin Mtei akizungumza na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama hicho, Mh. Edward Lowassa wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Kamandolu, leo Agosti 15, 2015, kulikofanyika Mkutano wa kumtambulisha.
Muasisi Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mzee Edwin Mtei akizungumza na maelfu ya wananchi wa Jiji la Arusha, wakati akimtambulisha Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama hicho, Mh. Edward Lowassa, wakati wa Mkutano wa kutafuta udhamini wa Tume ya Uchaguzi na kutambulishwa kwa Mgombea huyo na Mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Kimandolu, leo Agosti 15, 2015.
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Mh. Godbless Lema akihutubia wananchi kwenye Mkutano wa hadhara wa kutafuta wadhamini wa Tume ya Uchaguzi wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa,pamoja na kutambulishwa kwa wananchi, uliofanyika Agosti 15, 2015, kwenye Uwanja wa Kimandolu, Jijini Arusha.

KUONA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA AU BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. hahahahahahahahahahha naanza kwa kucheka, ok kwanza tuliona Dar kisha mbeya, leo arusha nachtaka kusema ni kwamba iwapo mafuriko haya yataendelea kwa mikoa mitatu tu ijayo yaani Mwanza, Kigoma na Dodoma basi sioni sababu ya kuhariku karatasi , muda na fedha kwa kufanya uchaguzi si lazima kugenza wengine twaweza mkabidhi mtu ikulu bila ya box la kura kwa hali hii kuna nini tena kilichobaki.

    ReplyDelete
  2. Mnajidanganya hata chui ana vas ngozi ya kondoo vilevile kama unaelewa msemo huo basi nyie pigeni kimya mkikesha na kuomba maajabu ya tokee si vinginevyo, kwa maana sio wote waliovalia vazi la chadema ni chadema wapo wanafiki ambao wanakujidai ni ukawa lakini ni ccm damu hawataki kukata mfereji wao wa kupata riziki kumbuka KURA NI SIRI YAKO SIO WINGI WA WATU HATA MREMA WAKATI YUPO NCCR ALIJAZA WATU NYOMI NA ALIISHIA KUANGUKIA PUA. TAFAKARI NENO LA LEO.

    ReplyDelete
  3. Hayo mafuriko yakiendelea mimi napenda kuwashauri wadau waanze kununua life vest wasije kuzama na mafuriko yao. Na kama haujui kuogolea basi kimbilia kwenye jahazi ya CCM.
    CCM ndio tumaini la kupona na hilo balaa la mafuriko

    ReplyDelete
  4. Nape lazima aelewe kuwa mafuriko hayawezi kuzuiwa kwa mikono...hahahah

    ReplyDelete
  5. Niwakati wa mabadiliko lazima ukawa wachukue nchi....ccm give orthers chance tuone na wao watafanya nini.....yenu tumesha yaona...umaskini wa raia ulio kithiri...madini tunayo...makaa ya mawe tunayo...mbuga za wanyama tunazo...urenium tunayo gesi tunayo....mageuzi muhimu

    ReplyDelete
  6. We have been there before.Wakati tulipokuwa tunasukuma gari la bwana Lyatonga Mrema.

    ReplyDelete
  7. Namba itahesabiwa na kutangazwa na Tume ya uchaguzi kutokana na kura za kwenye debe sio kwenye mikutano ya hadhara, ingekuwa ni mikutano CCM ingeshaapisha mgombea wake, Oktoba haiko mbali matokeo ya debe yataongea.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...