Mhe. Jaji Ferdinand Wambali (aliyesimama), Mkuu wa Chuo cha Mahakama  Lushoto (IJA),akitoa mada juu ya utendaji kazi katika Mahakama katika mafunzo yaliyoanza kufanyika mapema leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa (JNICC) jijini Dar es Salaam.
 Mhe. Shaban Ali Lila, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania (katikati) akitoa neno la utangulizi katika Semina ya Mafunzo elekezi kwa Wahe. Majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania walioapishwa hivi karibuni, aliyeketi kushoto ni Mhe. Anold Nsekela, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani (T) kulia ni Mhe. Salvatory Bongole, Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Mhe. Shaban Ali Lila, Jaji Kiongozi- Mahakama Kuu ya Tanzania (katikati) Mhe. Anold Nsekela, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani (T), Mhe. Salvatory Bongole, Kaimu Jaji Mfawidhi-Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja na Wahe. Majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania walioapishwa hivi karibuni, Majaji hao wapo katika mafunzo elekezi yenye lengo la kuwawezesha sheria mbalimbali na taratibu za Kimahakama. Mafunzo haya yataendelea kufanyika katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto (IJA) kuanzia tarehe 24.08.2015 ambapo mada mbalimbali zitatolewa ili kuwawezesha Wahe. Majaji hao kuifahamu Mahakama, ikiwa ni pamoja na misingi  na taratibu za utoaji huduma ya haki nchini. (Picha na Mahakama).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...