Na  Bashir  Yakub 

Kumbambikiza   mtu kesi  ni  kosa. Si  tu  ni  kosa  bali  pia  ni  kinyume  kabisa cha  haki  za  binadamu  na ustaarab wa  dunia. Inawezekanaje  mtu  akashtakiwa  kwa  kosa  ambalo   si  tu  hakulitenda  bali  pia  halijui  kabisa. Ni  matendo  yanayofanywa  na  watu  makatili  na  mabazazi.  Niseme  tu  mapema  kuwa  kosa  hili  haliwahusu  tu  askari  isipokuwa  kila  mtu   ambaye  anaweza  kumshtaki  mwingine  kwa  kosa  ambalo  anajua  kabisa  halikutendeka  au  lilitendeka  lakini  anayeshitakiwa  siye  aliyelitenda. 

1.NINI  MAANA  YA  KUBAMBIKIZA  KESI.

Kwa  jina  la  kitaalam  kubambikiza  kesi  huitwa  “malicious  prosecution”. Kwa  tafsiri  ya  kiswahili  ya  moja  kwa  moja  ni  “kushitaki  kwa  hila”. Linatumika  neno  kubambikiza  kesi  kwakuwa  ndilo  lililozoeleka  na  kufahamika. 

 Maana  ya  kubambikiza  kesi  ni  kumfungulia  mtu  kesi  ya  jinai  kwa  hila  na  bila  sababu  za  msingi  lakini  mtu  huyo  aliyeshitakiwa akashinda hiyo kesi. Kwa  tafsiri hii  tunapata  kujua  kuwa  kubambikiza  kesi  kunahusisha kushtakiwa  kwa  kesi  za  jinai. Kwahiyo  kusingiziwa  kutenda  jinai  ndio  kubambikizwa  kesi.  Jinai  ni  kama  kushtakiwa  kwa  wizi,  ukabaji, ubakaji, udhalilishaji, kutusi, kuharibu  mali, kupigana, kukutwa  na/au  kujihusisha  na  dawa  za  kulevya  ikiwemo  bangi, kuua,  kujaribu  kuua  au  kujiua, kula  njama , utapeli,  na  mengine  mengi. 

Ukisingiziwa  kutenda  haya   na  ukashitakiwa  basi  unakuwa  umeingia  katika  maana  ya  kubambikizwa  kesi.

2.  TABIA  YA  ASKARI  KUWAMBIKIZIA  KESI  RAIA.

Jamii  imelalama  sana  kuhusu  hili. Leo  si  ajabu  bodaboda   akazozana  na  askari  kuhusu  labda  ukiukaji  wa  taratibu  za  barabarani   lakini  akafikishwa  kituoni  akaambiwa  aoneshe  bunduki  ilipo. Au  mtu  akakamatwa  kwa  kosa  la  ugomvi   akafikishwa  kituoni  akaandikiwa  kosa  la  kukutwa  na bangi. Na  mambo  mengine  yanayofanana  na  hayo. Jamii  imekuwa  haina  amani  na hili  limelegeza  sana  uhusiano  wa  jeshi   la  polisi  na  wanajamii. 

Utafiti  unaonesha  kuwa   hali  hii  imekuwa ikijitokeza  hasa  pale ambapo askari  amekosana  na  mtu   pengine  umejitokeza  ubishi   wakati  raia  akikamatwa au vinginevyo ambapo  askari  hufanya hivi  kuonesha  kwamba   anaweza.  Zaidi  baadhi  ya  watu  hasa  wenye  fedha  wamekuwa wakitumia  njia  hii kuwakomoa  au  kuwatia   adabu  wabaya  wao. Askari  anatanguliziwa  kidogo  linatengenezwa  kosa,  mtu  anakamatwa  na  kushitakiwa. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mbali na matumizi mabaya ya madaraka na hujuma, tatizo pia ni mahakimu, majaji na waendesha mashtaka wasiokuwa huru na wakosa busara kwa kuruhusu kesi kama hizo kufunguliwa. Kesi kama hizo huitwa "frivolous or Vexatious litigation". Ni njia inayotumiwa na watu na serikari nyingi hasa za Afrika na Asia zenye kukandamiza wananchi wake hasa wale wanaoonekana kama ni wapinzani. Katika nchi zenye Uhuru wa mahakama na uongozi bora wa kisheria, Mahakimu na majaji hutoa adhabu kwa watu, wanasheria na waendesha mashtaka wanaofungua kesi kama hizo. Kuwepo kwa kesi nyingi za aina hiyo ni ushahidi wa nchi kutokuwa na uongozi bora wa kisheria na pia udhaifu wa mahakama. Jo Sheffu, dar

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...