Na Bashir Yakub
Kumbambikiza mtu kesi ni kosa. Si tu ni kosa bali pia ni kinyume kabisa cha haki za binadamu na ustaarab wa dunia. Inawezekanaje mtu akashtakiwa kwa kosa ambalo si tu hakulitenda bali pia halijui kabisa. Ni matendo yanayofanywa na watu makatili na mabazazi. Niseme tu mapema kuwa kosa hili haliwahusu tu askari isipokuwa kila mtu ambaye anaweza kumshtaki mwingine kwa kosa ambalo anajua kabisa halikutendeka au lilitendeka lakini anayeshitakiwa siye aliyelitenda.
1.NINI MAANA YA KUBAMBIKIZA KESI.
Kwa jina la kitaalam kubambikiza kesi huitwa “malicious prosecution”. Kwa tafsiri ya kiswahili ya moja kwa moja ni “kushitaki kwa hila”. Linatumika neno kubambikiza kesi kwakuwa ndilo lililozoeleka na kufahamika.
Maana ya kubambikiza kesi ni kumfungulia mtu kesi ya jinai kwa hila na bila sababu za msingi lakini mtu huyo aliyeshitakiwa akashinda hiyo kesi. Kwa tafsiri hii tunapata kujua kuwa kubambikiza kesi kunahusisha kushtakiwa kwa kesi za jinai. Kwahiyo kusingiziwa kutenda jinai ndio kubambikizwa kesi. Jinai ni kama kushtakiwa kwa wizi, ukabaji, ubakaji, udhalilishaji, kutusi, kuharibu mali, kupigana, kukutwa na/au kujihusisha na dawa za kulevya ikiwemo bangi, kuua, kujaribu kuua au kujiua, kula njama , utapeli, na mengine mengi.
Ukisingiziwa kutenda haya na ukashitakiwa basi unakuwa umeingia katika maana ya kubambikizwa kesi.
2. TABIA YA ASKARI KUWAMBIKIZIA KESI RAIA.
Jamii imelalama sana kuhusu hili. Leo si ajabu bodaboda akazozana na askari kuhusu labda ukiukaji wa taratibu za barabarani lakini akafikishwa kituoni akaambiwa aoneshe bunduki ilipo. Au mtu akakamatwa kwa kosa la ugomvi akafikishwa kituoni akaandikiwa kosa la kukutwa na bangi. Na mambo mengine yanayofanana na hayo. Jamii imekuwa haina amani na hili limelegeza sana uhusiano wa jeshi la polisi na wanajamii.
Utafiti unaonesha kuwa hali hii imekuwa ikijitokeza hasa pale ambapo askari amekosana na mtu pengine umejitokeza ubishi wakati raia akikamatwa au vinginevyo ambapo askari hufanya hivi kuonesha kwamba anaweza. Zaidi baadhi ya watu hasa wenye fedha wamekuwa wakitumia njia hii kuwakomoa au kuwatia adabu wabaya wao. Askari anatanguliziwa kidogo linatengenezwa kosa, mtu anakamatwa na kushitakiwa.
Mbali na matumizi mabaya ya madaraka na hujuma, tatizo pia ni mahakimu, majaji na waendesha mashtaka wasiokuwa huru na wakosa busara kwa kuruhusu kesi kama hizo kufunguliwa. Kesi kama hizo huitwa "frivolous or Vexatious litigation". Ni njia inayotumiwa na watu na serikari nyingi hasa za Afrika na Asia zenye kukandamiza wananchi wake hasa wale wanaoonekana kama ni wapinzani. Katika nchi zenye Uhuru wa mahakama na uongozi bora wa kisheria, Mahakimu na majaji hutoa adhabu kwa watu, wanasheria na waendesha mashtaka wanaofungua kesi kama hizo. Kuwepo kwa kesi nyingi za aina hiyo ni ushahidi wa nchi kutokuwa na uongozi bora wa kisheria na pia udhaifu wa mahakama. Jo Sheffu, dar
ReplyDelete