Na Bashir Yakub
Hapa kwetu Tanzania tunazo ndoa za aina kuu mbili. Kwanza tunazo ndoa za kiraia au kiserikali, na pili tunazo ndoa za kimila.
Ndoa za kiraia au za kiserikali kama zinavyojulikana kwa wengi ni zile ambazo hufungwa chini ya usimamizi wa mamlaka za serikali kama ofisi ya mkuu wa wilaya n.k. Na kwa upande wa ndoa za kimila hizi ni zile ambazo hufungwa kutokana na taratibu za watu wa kabila au koo fulani kwa mujibu wa tamaduni na desturi zao. Ndoa za kimila hujumuisha pia ndoa zinazofungwa kwa taratibu za kidini.
Kwa taratibu za kidini tunapata ndoa nyingi kwa mfano ndoa zinazofungwa kwa mujibu wa mafundisho ya kiislam, ndoa zinazofungwa kwa mafundisho ya kikristo, budha , wahindu na dini nyingine pia wanazo taratibu zao.
Aidha sehemu za kufungia ndoa kisheria ni maeneo ya nyumba za ibada, kwenye ofisi za serikali, ubalozini kwa walio nje ya nchi, majumbani na sehemu nyingine ambazo ni wazi kwa watu kushuhudia. Pamoja na hayo yote juu yafaa tujue kuwa zipo aina za ndoa au mahusiano yaliyokatazwa kabisa kuitwa ndoa.
Juu ya hilo sheria imeainisha mambo ambayo yakifanywa au yakipitiwa ndoa inakuwa halali halikadhalika yale ambayo yakifanywa au kutofanywa ndoa inakuwa haramu.Haya ni mengi isipokuwa hapa tutaona baadhi yake. Pamoja na hayo kabla ya kuyaona hayo kwanza tuangalie baadhi ya taratibu za kupitia kabla ya kuendea suala la kufunga ndoa.
1.BAADHI YA MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA KUFUNGA NDOA.
( a ) Kifungu cha 28 cha sheria ya ndoa kinasema kuwa ikiwa ndoa itafungwa katika ofisi za wilaya, kwenye nyumba za ibada au popote kwenye jamii basi ni vema ikawa ruhusa kwa wanajamii au waumini wa nyumba hiyo ya ibada kushuhudia bila kuzuiwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...