TWAWEZA inatangaza uzinduzi wa midahalo iitwayo Mkikimkiki 2015. Midahalo hii imeanzishwa ili kutoa fursa na jukwaa kwa vyama vya siasa kunadi sera zao kwa wananchi. Aidha midahalo hii tawapa wananchi fursa ya kuwahoji na kuwapima wagombea na wataalamu wa vyama vikuu vya siasa.
Mfululizo huu wa midahalo umekuja wakati muafaka. Utafiti ulidhaminiwa na Twaweza, uligundua kuwa wananchi 8 kati ya 10 wanafikiri kuwa wagombea ubunge (78%) na urais (79%) wanapaswa kuwa na midahalo ya pamoja. Mbali na mikutano ya hadhara ya kampeni, wananchi wana nafasi finyu sana ya kuwasikiliza na kuwahoji wagombea na vyama vya siasa kuhusu mitazamo, ilani na sera zao katika nyanja mbalimbali.
Maswali ya wananchi na majibu ya hapo kwa hapo ni fursa muhimu kwa wote kupanua uelewa wa wote kuhusu sera na mipango hiyo.
Wananchi wote wanakaribishwa kuwasilisha maswali yao kupitia mtandao na ujumbe mfupi wa simu (SMS). Vilevile, washiriki wa mdahalo na watazamaji wataweza kuuliza maswali wakati wa midahalo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...