Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bi.
Rehema Mkamba akikabidhi msaada wa vifaa
vya ujenzi vilivyotolewa na LAPF kwa
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo.
Mwalimu mkuu wa shule ya Sekondari Dodoma Ndugu Marco Masala akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya msaada wa vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na LAPF.
Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bi. Rehema Mkamba akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya msaada wa vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na LAPF
Baadhi ya Wanafunzi wa Dodoma Sekondari waliohudhuria hafla hiyo.
Mwanafunzi wa kidato cha sita Sabina John akitoa neon la shukurani kwa niaba ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Dodoma.
Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo hii
unakabidhi msaada wa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shillingi millioni
mbili kwa uongozi wa Shule ya Sekondari Dodoma kwa ajili ya ujenzi wa
uzio,baada ya kupokea ombi la kuchangia ujenzi huo.
LAPF inaamini kuwa msaada huu
utasaidia kuchangia gharama na hatimaye kufikia lengo la kukamilisha ujenzi huo
na kuhakikisha usalama wa wanafunzi. Msaada huu utawanufaisha si tu Wanafunzi na Walimu wa Shule ya Sekondari Dodoma bali pia
wadau wengine mbalimbali ambao wamekuwa wakitumia viwanja vya Shule hii kwa
michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na watumishi wa LAPF.
LAPF imekua ikitoa misaada mbalimbali
ya kijamii hasa kwa wadau muhimu kama Shule za Msingi na Sekondari,Vituo vya
Afya, Vituo vya Watoto yatima , kuchangia michezo nk.
LAPF ni Mfuko wa Pensheni ambao pamoja na majukumu mengine, jukumu lake kuu ni
kutoa mafao ya Pensheni kwa wanachama wake. Mafao yanayotolewa na LAPF ni
pamoja na;
·
Pensheni ya Uzeeni.
·
Pensheni ya Ulemavu.
·
Pensheni ya Urithi.
·
Fao la Uzazi.
·
Mikopo ya kujikimu.
·
Mikopo ya elimu .
·
Mikopo ya nyumba.
·
Mikopo kwa wanachama wa kupitia Saccos.
·
Mikopo kwa Wastaafu.na
·
Msaada wa mazishi.
Kwa sasa Mfuko wa pensheni wa LAPF unaandikisha
wanachama kutoka sekta zote kama vile Waalimu, Watumishi wa Afya, Wajasiliamali
nk.
MAISHA
POPOTE NA LAPF
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...