Mkuu wa usalama Barabarani Kanda Maalum Dar es Salaam, Peter Sima katikati akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya Maonesho ya usalama barabarani ya yatakayofanyika tarehe Agosti 24 na 25 mwaka huu katika viwanja vya mashujaa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, kulia ni Mrakibu Mwandamizi wa Polisi na Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Kinondoni, Awadhi Haji na kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama barabarani, Elifadhili Mgonja.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama barabarani, Elifadhili Mgonja.
Picha na Emmanue Massaka.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
AJALI
za barabarani jijini la Dar es Salaam zimepungua katika kipindi
cha nusu ya kwanza ya 2015 ikilinganishwa na kipindi kama hicho kwa
2014.
Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti
wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Dar es Salaam, Elifadhili Mgonja
amesema kuwa takwimu zinaonyesha kupungua kwa ajali za barabarani 2,731
katika kipindi cha Januari -Juni 2015 zilitokea ajali za vifo 1,731
ikilinganishwa na ajali 4,462 zilizotokea kipindi cha Januari-Juni ,2014
ambayo ni sawa na upungufu wa asilimia 61.
Amesema kuwa ajali za
vifo 87 katika kipindi cha Januari hadi juni mwaka 2015 zimeripotiwa
kwa ajali za vifo 165 ikilinganishwa na ajali za vifo 252 zilizotokea
katika mwaka uliopita ambayo sawa na asilimia 34.5.
Mgonja amesema
idadi ya watu waliokufa 93 kwa 2015 katika na idadi ya ajali zilizokuwa
187 kwa ikilinganishwa na watu waliofariki 280 katika mwaka uliopita
sawa na asilimia 33.2.
Amesema upungufu waliojeruhiwa 1, 801 kwani
mwaka huu ,waliojeruhiwa walikuwa 1,650 ukilinganishwa na mwaka uliopita
wa mwaka 2014 uliokuwa na majeruhi 3,451 sawa na asilimia 52.18.
Aidha
amesema kuwa wataandhimisha wiki ya usalama barabarani mkoa wa Dar es
Salaam kuanzia Agasti 24 hadi 28 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini
Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...