Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja akizungumza na waandishi wa (habari hawapo pichani )juu ya kungatuka katika chama hicho na kujiunga na Chadema leo katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo jijini Dar es Salaam, Kulia ni John Gudinita.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, John Gudinita akitangaza kujiuzuru katika chama hicho na Kujiunga na Chadema leo majira ya saa tano katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo jijini Dar es Salaam. kushoto Sheik Rajab Katimba na kulia ni Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja.
Aliyekuwa.Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Shinyanga,Hamis Mgeja akionesha kuwa yeye ni chandema kwa sasa.
Wandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa CCM,Mkoa wa Shinyanga,Hamis Mgeja wakati akitangaza kujiuzuru katika chama hicho na Kujiunga na Chadema leo majira ya saa tano katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja amengatuka uanachama wa CCM pamoja kujiuzuru nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam,Mgeja amesema kuwa ametafakari sana na kuona aungane na chama hicho.
Mgeja amesema kuwa anaondoka kwenda kutafuta mabadiliko katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kuongeza kuwa wametumikia chama hicho kwa muda mrefu lakini sasa imefika wakati wa kuondoka.
Aidha amesema kuwa CCM ya sasa imekuwa na vitu ambavyo vinafanywa na watu baadaye kuikigharimu chama kutokana na kuacha msingi wa kukubali maoni ya wanachama.
Wakati huo huo katika mkutano huo aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam,John Guninita naye amengatuka katika chama hicho na kujiunga ba Chadema kuongeza nguvu Ukawa.
Guniinita amesema kuwa sasa umefika wakati wa kuondoka kutokana na Chama kuacha kusikiliza wanachama wake na badala yake kuendeleza chuki ndani ya Chama.
mhhh . ...kaazi kweli kweli!
ReplyDeleteMimi sitoki hata kama sipati kitu( nakufa na tie shingoni)
ReplyDeleteThe mdudu, ogopeni sana watu kama hao mwangalieni kwajinsi alivyo nenepeana ndani ya CCM kwa Rushwa na bado hajakoma anaenda kuongeza unene Chadema na Ukawa mimi nilijua labda wanatangaza kujiuzuru kutokana umri wao kumbe sivyo kabisa mimi ningependa kama Ukawa wakishindwa 2015 mizigo kama hii wafilisiwe mari zao za Rushwa.
ReplyDeleteHawa jamaa wanapokea kila kitu toka chama tawala, kazi kwelikweli
ReplyDeleteNatumaini huyo mdau hapo juu ana ushahidi wa hizo rushwa anazotuambia, kama hana basi yeye ni bua. Anaweza kufikishwa mahakamani na kunyolewa nywele.
ReplyDeleteTazama jambo hili, kuwa tangu kuzaliwa kwa chama hapajatokea mambo kama haya.Watu wanakero fulani fulani za chama na the right action for the chama ni kuunda kamitii na kuchungua ukorofi huo, siyo kuwazomea wanaowacha chama.
"The Mdudu", ni vizuri uwe na uhakika wa ki-ushahidi (tena pasipo shaka yoyote) ikiwa kwa namna yoyote ile afya za hao ndugu zina uhusiano wowote na rushwa. Tuache ushabiki, kuhana toka chama kimoja kwenda kingine ni utashi wa mtu. Sasa utasemaje ikiwa watu haohao baada ya muda watarudu sisiemu?
ReplyDeleteGuninita ni malaya kisiasa
ReplyDeleteUmeua, tupe ufafanuzi
Delete