Tume ya Taifa ya uchaguzi Makao makuu, hapo kesho inatarajiwa kupokea fomu za uteuzi za vyama 13 kwa ajili ya uteuzi wa nafasi ya kugombea urais kwa ajili ya uchaguzi mkuu ambao utafanyika hapa nchini mwezi oktoba mwaka huu. 
 Akizungumza katika mkutano wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na wawakilishi kutoka katika madhehebu ya dini hapa nchini katika hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam leo, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damiani alisema uchaguzi mkuu wa Mwaka huu utahusisha majimbo mapya 25 na kata 620 ambazo zimeongezeka kutokana na sababu za kiutawala na kuongezeka kwa Idadi ya watu. 
 Aidha Jaji Lubuva alisema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, imeandaa mkakati na mongozo wa kutumia radio na televisheni za kijamii zikiwemo zile za dini kutoa elimu kwa wapiga kura katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi mkuu ili kuelimisha wapiga kura kuhusiana na uchaguzi huo. Katika mkutano huo, Jaji Lubuva amewataka viongozi wa dini kutoonyesha hisia za kuegemea upande wowote au kutowashawishi waumini wao kuegemea upande wowote hasa wanapoto elimu ya mpiga kura ili uchaguzi ufanyike kwa uhuru na Amani. 
 “Tume inawataka mnapotoa mafundisho kutoonyesha hisia za kuwa upande wowote wa chama chochote cha siasa na zaidi kuepuka kushawishi waumini wenu kuegemea upande wowote au mgombea” alisema Jaji Msaafu Lubuva na kuongeza kuwa Tume ya Taifa ya uchaguzi inawaomba viongozi wa dini kuyatumia majukwaa yao kuwaelimisha waumini waweze kufanya kufanya maamuzi sahihi. 
 Akiwaslisha mada katika mkutano huo,Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kailima Ramadhani alisema kuwa azma ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni kuhakikisha kwamba kila raia mwenye sifa na aliyejiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura anapata fursa ya kushiriki katika uchaguzi na kuhakikisha kuwa uchaguzi huo unakuwa wa wazi, huru na haki ili kujenga demokrasia na kukuza uatwala bora hapa nchini. 
 Ramadhani aliongeza kuwa, hadi sasa,Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekamilisha mambo kadhaa katika kufanikisha uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu. 
Baadhi ya mambo ambayo yamekamilika hadi sasa ni pamoja na uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, na kuweka wazi daftari la awali la wapiga kura. Uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu nchini Tanzania utashirikisha jumla ya majimbo 264 na kata 3,957 kutoka Tanzania Bara. 

+255(0)772 55 55 53
LISTEN LIVE
http://myradiostream.com/focusradiotz
Tume ya Taifa Ya Uchaguzi Tanzania
YOUTUBE / TV
http://bitly.com/1Leujup
VIPINDI VYA REDIO
http://bitly.com/1Clt0r8 
FACEBOOK
http://bitly.com/1zIiIkq 
TWITTER
http://bit.ly/1678Vq2




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...