Mgombea ubunge jimbo la vunjo
kupitia chama cha TLP Agustino Mrema (kushoto) akipokea fomu ya kugombea
ubunge katika jimbo la vunjo kutoka kwa mkurugenzi wa halmashauri ya
moshi vijijini FOLGENCE MPONJI(Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
………………………………………………………………………………..
MGOMBEA ubunge jimbo la Vunjo
na mwenyekiti wa chama cha TLP ,Agustino Lyatonga Mrema ametamba kuwa
jimbo hilo ni mali yake na hayuko tayari kuona likichukuliwa na
manyang’au aliodai wa Ukawa.
Mrema alitoa kauli hiyo wakati
akiongea na mamia ya wafuasi wa chama hicho muda mfupi baada ya kuchukua
fomu ya kugombea kiti hicho katika ofisi cha halmashauri ya wilaya ya
Moshi Vijijini.
Mrema alisema kuwa jimbo la
vunjo ni mali yake na hayupo tayari kuliacha lichukuliwe na manyang’au
wa ukawa ambao alidai ni wanyang’anyi.
Alisema amelazimika kuchukua
fomu ya kugombea jimbo hilo kutokana na maombi ya wananchi wa jimbo la
vunjo wengi wao wakiwa wanawake ambao muda mwingi walikuwa wakimfuata
nyumbani kwake wakimtaka agombee kutokana na rekodi nzuri aliyo watendea
kipindi kilicho pita,
Hata hivyo alieleza kuwa
propaganda zinazo enezwa na wapinzani wake wakidai kuwa yeye amezeeka na
ni mgonjwa, nizakupuuzwa kwani kwa sasa yeye ana afya njema na anataka
aitwe ‘bebi’ huku akionya kuwa wanao tumia sera ya uzee na ugonjwa kwa
lengo la kumwangusha kamwe hawatafanikiwa kwani wananchi wa vunjo pamoja
na mkewake ,Rose Mrema ndio wenye kujua utendaji wake wa kazi na hivyo
hwahitaji kuchaguliwa mtu mwingine.
“ Mengi yamesemwa kuwa mrema
hagombei ni mzee ni mgonjwa hivi mkiniona mimi ni mzee jamani ,mimi ni
bebi ,uzee mwisho Chalinze ,waliokuwa na wasiwasi eti sigombei .sasa
nagombea afya yangu imeimarika na hao ukawa wataisoma namba mwaka
huu”alitamba Mrema
Mrema alisema kuwa kazi aliyo
ifanya katika kipindi chake cha ubunge inaonekana na amejipanga
kuhakikisha wananchi wa jimbo hilo wananufaika zaidi na juhudi zake
kwakuwa amekuja na kasi mpya ya kuwaletea maendeleo na tayari amenunua
gari la kusafirisha abiria (coster) linalotumika katika jimbo hilo
kusafirisha wakina mama wajawazito, shughuli za misiba pamoja na kubeba
wananchi katika maeneo yao bila kuwatoza malipo yoyote
,
Hata hivyo mremna
anaonekana kukubalika zaidi na akina mama ambao walidai kuwa Mgombea
huyo amekuwa akiwapigania akiwa bungeni ili wapatiwe mikopo ya bei nafuu
pia amenunua gari la abilia kwa ajili yao
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...