Selemani Rashidi (kushoto), akiwa na mama yake mzazi pichani, ambaye alisimulia mkasa mzima wa mwanaye, alizaliwa akiwa mzima na baada ya kuzaliwa alipatwa na matatizo ya ugonjwa wa Degedege na alimpeleka kwa mganga wa kienyeji na kupona matatizo hayo na ndipo kikaota kipele kichwani cheusi na kikawa kinakuwa na kushikana na sikio, kutokuwa na uwezo wa kipesa hakuweza mpeleka popote, Baba yake yapata Miaka kumi na tano toka afariki na ukizingatia ni pesa inayo hitajika, hayo yalisemwa na mama yake mzazi ambaye anaitwa Zamda Kibosha, wakiwa wamekaa kwao maeneo ya kitongoji cha Lugongoni, (A) Kataa ya Nguruka Wilaya ya Uvinza Mkoa wa Kigoma, Mama yake anasema mwanaye baada ya kuota kinyama hicho, kauli kutoka ni kwa shida, akijibu maramoja harudii tena kuongea na chooni anakwenda mwenyewe na kula anakula kama kawaida, mama anaomba kwa mtu yoyote mwenye kuona na kusia anaomba msaada wa hali na mali ili mwanaye apate matibabu, kwa mawasiliano mwenye chochote kitumwe kwenye namba 0687946492, Mariam Hamza Thabiti, Nguruka kigoma. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA) Mmiliki wa ujijirahaa blog.
Selemani Rashidi, Namba msaada kwa yeyote anisaidie niweze kufanyiwa matibabu kwa kinyama kilicho jitokeza kichwani mwangu toka nilipo zaliwa.
Selemani Rashidi, anapoishi na mama yake mzazi
Sub'hanallah! Pole sana Selemani na pole sana Mama kwa kuuguza. In Sha Allah kwa uwezo wake Mwenyeez Mungu atajaaliya 'shifaa' na kwa wale walioguswa na hili na hali zao kiuwezo zinawaruhusu, basi jamani kutowa ni moyo na kesho mtayakuta malipo yenu huko usoni twendako. Inatilisha imani na kusikitisha sana. Mola awajaaliye kupitia wasamaria wema, mfanikiwe na kukamilisha tiba zote juu ya hilo. In Sha Allah.
ReplyDeletePole Sele, ndo maana mimi sijamwita na sintomwita mtu yeyote yule "mheshimiwa", wote nawaita Ndugu Fulani. Naomba msaada wa kumsaidia Sele utoke SERIKALINI. Kwani Sele ni mtanzania! kama Hospitali za Tanzania hawawezi kumpatia tiba, basi apelekwe Nje ya nchi kama ambavyo watanzania wengine wengi tu ambao walipelekwa nje ya nchi kwa matibabu, au huduma hii ni ya "Waheshiwa" tu?
ReplyDeletePole sana Ndugu Selemani...dah nimeumia sana kukuona upo katika hali hii. Mwenyezi Mungu akuponye ndugu yangu. Inauma sana kuona raia kama huyu (na wengine wengi tu)wanaugua magonjwa kama haya na serikali inashindwa kuwapatia tiba raia wake hawa maskini. Ndugu selemani ni mmoja tu kati ya raia wengi waliopo vijijini Tanzania wanaogua kwa mateso bila msaada wa serikali. Hivi kweli kwa zaidi ya miaka 50 na utajiri wote tunaoambiwa tunao Serikali kweli imeshindwa kumtibu ndugu Selemani?nini basi maana ya kuwa proud ya kuwa raia wa tz?mbona serikali za nchi nyingine zipo tayari hata kuingia vitani raia wake mmoja tu anapotekwa au kupata matatizo nje ya nchi?je serikali ya tz imeshindwa kweli hata hili la ugonjwa tu?
ReplyDeleteAnkali naomba sana usibane hii msg ili wahusika waione na Mungu mwenyezi atakuongezea. Hivi kweli tuna raha gani viongozi wetu kutumia mabilioni kwenye sherehe na magari ya anasa wakati kuna wakina ndugu Selemani wengi tu wanaohitaji kidogo sana wanachokitumia?hivi kweli miaka zaidi ya 50 bado hali ipo hivi?inauma sana kwa kweli..ndugu yangu Selemani nitakuombea Mungu akuponye.
mdau
Sweden