Na Sensei Rumadha Fundi
Mara nyingi neno”Meditation” au kutafakari huchanganywa  na kufikiri ni kukaa kimya kufumba macho kiufanisi au kuwaza jambo fulani. Pia, wengine huchanganya hili neno na kuwa umekaa kimya na kujaribu kutofikiria lolote, ama pia kuivuta au kuisukuma akili yako na kutoku fikiria kitu cha iana yeyote ile muda wote wa kutafakari na kuamini kwamba hiyo ni “Meditation” au Tafakari. Kamwe, hamna hata moja ya mifano hii inaweza kuifikia maana yake halisi katika mfumo kisayansi na filosofia ya “Yogic”.

Kisayansi ya Yoga, “Meditation” inaitwa “Mtiririko wa akili”( Flow of the mind).” Kuiongoza akili au mawazo ya mtu kupia Meditation, inahitaji pointi au sehemu muhimu katika maungo yako unayo kuwa unatumia kama vile mfano wa mionzi ya akili kuirushia na kuelekeza katika sehemu moja tu. Hivyo kwa kutumia msaada wa sauti maalum itwayo “Mantra”, hiyo ndio chombo hutumika kupitia mkufunzi aliye hitimu  Sanaa ya Yoga na kufundisha kutokana na mazingira tofauti kati ya tofauti za watu zilivyo.


Kama jinsi inavyoelezwa katika filosofia ya Yoga kwamba, akili ya mwana adam, kamwe  haitulii, wakati wote ipo mbio na inatafuta cha kufikiri, hivyo basi huwa ni kazi ngumu sana kwa mtu hata kuanza tu somo la kwanza (First lesson), kwa mistuko ya mchanganyiko wa mawazo ya mwana adam. Hivyo huwa taabu sana kukusanya mawazo yako binafsi na kufanya meditation bila muongozo wa kiutaam.
Napenda kuongelea vitu vichache hapa. Kuna vitu, au pointi tano tofauti zilizo muhimu na utumika katika mbinu za kutafakari kwa jina la “Sense withdrawal”, ambayo huitajika ili uweze kushawishi akili yako na mawazo kwamba utaweza kutafakari bila vikwazo vya mawzo yoyote au kuwa na utata katika mfomo mzima wa kutafakari. Ufuatao ni muktasari tu wa jinsi gani wana-Yoga wana tafakari kwa masaa mengi bila mgongano au (interraption) kupitia njia hii: 


 Mwalimu wa Yoga na Karate wa kimataifa aishiye Mareka ni Sensei Rumadha Fundi katika mazoezi tofauti ya sanaa ya Yoga, akielezea ni nini hasa maana ya kutafakari kwa njia ya sanaa ya Yoga.

Meditation & Mantra

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mazoezi ya kawaida yanafaida mwilini, lakini baadhi ya mafundisho hapa yanatoka kwenye imani za Asia, imani nyingine hapa nchini haziruhusu waumini wake kushiriki.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...