Naibu waziri wa maji Mhe Amos Makalla amekagua mradi mkubwa wa maji utakaohudumia wananchi wa mji wa Bunda na vijiji 13 vilivyopo karibu na chanzo na vitakavyopitiwa na bomba kuelekea mji wa Bunda
Kwa mujibu wa injinia Gantala Gantala mkurugenzi wa mamlaka ya maji musoma ambao ndiyo wasimamizi wa ujenzi wa mradi huo kwa niaba ya wizara ya maji ameleza kuwa mahitaji ya maji sasa kwa wananchi wa mji wa Bunda ni lita milioni 5 kwa siku wakati uzalishaji wa sasa maji ni lita milioni moja na laki mbili tu hivyo mradi huu umekusudia kuzalisha maji lita milioni 8 kwa siku na hivyo kumaliza kabisa tatizo la maji mji wa Bunda na vijiji 13
Mradi wa maji Bunda unagharimu fedha shilingi bilioni 8 na umetekelezwa kwa awamu nne na utakamilika mwishoni mwa mwezi Septemba
Aidha naibu waziri wa maji amemwagiza mhandisi wa maji wilaya ya Bunda kufanya usanifu wa vijiji vya Busimbwe, Bulamba na Mwiseni vilivyoko karibu na chanzo vipatiwe maji ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya waziri mkuu Mizengo Pinda aliyoitoa mwezi mei mwaka huu wakati wa maadhimisho ya wiki ya maji iliyofanyika Bunda
Amewataka wakandarasi wote wa mabomba kutoka katika chanzo na mkandarasi wa mabomba usambazaji mjini kukamilisha mradi mwezi septemba kama walivyohaidi
Naibu waziri wa maji Mhe Amos Makalla akiwa na Aliyekuwa mbunge wa Mwibara ndugu Kangi Lugola wakiwasikiliza watalaam wa mradi
Naibu waziri wa maji Mhe Amos Makalla akitoa maagizo
Naibu waziri wa maji Mhe Amos Makalla akitembelea mradi huo
Naibu waziri wa maji Mhe Amos Makalla katika ghala ya mabomba ya maji
Huyu jamaa anatufaa sana ilifaa awe waziri wa maji na sio naibu
ReplyDelete