Habari na picha na Editha Karlo,
wa Globu ya Jamii Kigoma

Mgonjwa huyo amezikwa jana jioni kwa tahadhari zote zihusuzo magonjwa hatari ya kuambukiza.
Nguo, vitanda, mashuka na vitu vyake vyote alivyokuwa akitumia wakati wa uhai wake vimechomwa moto mara tu baada ya mwili wake kuzikwa eneo la Masanga nje kidogo ya mji wa Kigoma.
(Picha zinaonesha hatua mbalimbali toka mwili wa marehemu ulipoondolewa na wataalamu waliovaa mavazi maalumu hadi mazikoni).
Akiongea na mtandao huu daktari wa wakimbizi kutoka shirika la kusafirisha wakimbizi kwenda nje ya nchi (IOM) Dkt. Beda amesema kuwa marehemu ameishi katika kambi ya wakimbizi ya Nyalugusu Wilayani Kasulu kwa muda wa miaka mitatu yeye pamoja na familia yake.


"Ilipofika tarehe juzi Agosti 8 hali yake ilizidi kuwa mbaya ndipo uongozi ulipoamua kumpeleka katika hospital ya mkoa maweni kwaajili ya matibabu zaidi" alisema Dkt Beda.
Naye Kaimu mganga mkuu wa hospital ya nkoa wa kigoma Dkt Shija Ganai amethibitishia mtandao huu kuwa walimpokea mgonjwa huyo na kumlaza katika wodi namba 8 ya Grade One.
Alisema kuwa usiku wa kuamkia leo hali ya mgonjwa ilizidi kuwa mbaya na damu zilizidi kuongezeka, na walipompima maralia alikuwa na joto la kawaida la nyuzijoto 36.
Dkt. Ganai ameeleza kuwa ilipofika alfajiri ya kuamkia leo mgonjwa huyo alifariki dunia. Amesema kwamba mpaka sasa bado haijadhibitishwa kama mgonjwa huyo amekufa kwa ugonjwa wa ebola japo alikuwa na dalili zote za ugonjwa huo.


Aliongezea kuwa hivi sasa madaktari, manesi pamoja na ndugu wote waliokuwa wanamuhudumia mgonjwa hivi sasa wapo chini ya uangalizi maalumu wa madaktari kwa muda wa siku 21.
Taarifa hizi ambazo tumezisikia BBC asubuhi hii ni vizuri zithibitishwe kabla ya kutolewa. Utoaji wake usimamiwe na wizara ya Afya. Hatua zilizochukuliwa zinaonyesha utayari wa kukabiliana na maradhi na lazima zipongezwe. Yaliyotokea nchi za Afrika magharibi ikiwamo vifo vya wengi, shule na biashara kufungwa kwa zaidi ya miezi sita ikiwa ni pamoja na nci zao kunyanyapaliwa yalikuwa yanatisha. Athari ya kutoa taarifa kama hizi kwa nchi kabla ya kuthibitishwa inaweza kuwa kubwa ikitokea kuwa haukuwa ugonjwa uliodhaniwa. Jambo hili lichukuliwe kwa uzito wake, sehemu iliyoathirika isaidiwe kwa hali na mali na serikali. Kudhibiti hali ili yaliyotokea Liberia na Sierra Leone tuepushiwe. Ee Mungu ibariki Tanzania.
ReplyDelete