Globu ya Jamii imepata taarifa kutoka Wilayani Ludewa kuwa kumetokea ajali ya gari katika kata ya Lugarawa ambayo imepelekea vifo vya watu watano leo mchana.
Taarifa zinasema marehemu walikuwa wakitoka Lugarawa kwenda Shaurimoyo wakati gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kutumbukia katika mto Lugarawa (kama ionekavyo pichani). 

Chanzo cha ajali hiyo bado kujulikana. 
Habari zaidi tutawaletea kadiri ya zitakavyopatikana.

Mungu aziliaze roho za marehemu mahali pema peponi
-Amina

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Poleni wafiwa. Wanaohusika na barabara waweke vizuio kuzuia ajali kama hii ya gari kuanguka mtoni siku zijazo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...