Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Morrice Oyuke (Kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam wakati akitangaza matokeo ya takwimu za Pato la Taifa kwa robo mwaka ya kwanza kuanzia mwezi Januari – Machi, 2015 ambayo yameonyesha kuwa thamani ya Pato la imekua na kufikia shilingi trilioni 21.9 ikilinganishwa na shilingi trilioni 18.6 ya robo mwaka ya kwanza ya mwaka 2014. Kushoto kwake ni Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa Daniel Masolwa wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Morrice Oyuke wakati akitangaza matokeo ya takwimu za Pato la Taifa kwa robo mwaka ya kwanza kuanzia mwezi Januari – Machi, 2015 ambayo yameonyesha kuwa thamani ya Pato la imekua na kufikia shilingi trilioni 21.9 ikilinganishwa na shilingi trilioni 18.6 ya robo mwaka ya kwanza ya mwaka 2014. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO).

Na: Veronica Kazimoto

Matokeo ya takwimu za Pato la Taifa kwa robo mwaka ya kwanza yaani kuanzia mwezi Januari – Machi, 2015 yameonyesha kuwa thamani ya Pato la Taifa imekua na kufikia shilingi trilioni 21.9 ikilinganishwa na shilingi trilioni 18.6 ya robo mwaka ya kwanza ya mwaka 2014.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Morrice Oyuke amesema takwimu hizo zimetayarishwa kwa kuzingatia marekebisho ya Takwimu za Pato la Taifa kwa bei za mwaka 2007.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...