Na Lorietha Laurence –Maelezo

Jeshi la Polisi nchini limesitisha maandamano ya wafuasi wa vyama vya siasa wakati wa kuchukua ,kutafuta  wadhamini, na kurejesha fomu za kugombea nafasi ya Urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam Naibu Inspekta Jenerali wa jeshi la Polisi Abdulrahman  Kaniki (pichani) amesema kuwa jeshi limechukua hatua hiyo kutokana na ukiaukwaji wa sheria za usalama barabarani uliojitokeza wakati wagombea wa vyama vya CHADEMA na CCM walipochukua fomu za kugombea Urais makao makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

 “Kwa sababu za kiusalama   Jeshi la Polisi linasitisha maandamano ya aina yoyote wakati wote wa zoezi la kuchukua fomu, kutafuta wadhamini  mikoani pamoja na zoezi la kurejesha fomu “ alisema Kaniki.
Aidha aliongeza kuwa jeshi la Polisi nchini linafanya utaratibu wa kuwakutanisha wadau wote wa siasa ikiwemo viongozi wa vyama vya siasa vinavyoshiriki katika uchaguzi Mkuu ili kuona namna bora ya kufanya uchaguzi katika hali ya amani na utulivu.
“Jeshi la Polisi halitasita kumchukulia hatua za kisheria mgombea, kiongozi, mfuasi au chama chochote cha siasa kitakachokiuka agizo hili,” alisema.

Hatua hiyo ya jeshi la Polisi nchini inatokana na baadhi ya wagombea wa nafasi za Urais kufuatana na kundi kubwa la wanachama, na wapambe wao wakati wa kuchukua fomu za kuomba kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi hivi karibuni na kuhatarisha usalama ikiwemo kufungwa kwa barabara na kusababisha baadhi ya shughuli za kijamii kusimama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Zengwe Hilo lishaanza lol!!!! Always is something dam!!!!!

    ReplyDelete
  2. kutapatapa tu......haitasaidia kitu ni sawa kuzuia mafuriko kwa mkono

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...