Na
Lorietha Laurence –Maelezo
Jeshi la Polisi nchini
limesitisha maandamano ya wafuasi wa vyama vya siasa wakati wa kuchukua
,kutafuta wadhamini, na kurejesha fomu
za kugombea nafasi ya Urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi
Oktoba mwaka huu.
Akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Naibu Inspekta Jenerali wa jeshi
la Polisi Abdulrahman Kaniki (pichani) amesema
kuwa jeshi limechukua hatua hiyo kutokana na ukiaukwaji wa sheria za usalama
barabarani uliojitokeza wakati wagombea wa vyama vya CHADEMA na CCM
walipochukua fomu za kugombea Urais makao makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
“Kwa sababu za kiusalama Jeshi la Polisi linasitisha maandamano ya
aina yoyote wakati wote wa zoezi la kuchukua fomu, kutafuta wadhamini mikoani pamoja na zoezi la kurejesha fomu “
alisema Kaniki.
Aidha aliongeza kuwa jeshi
la Polisi nchini linafanya utaratibu wa kuwakutanisha wadau wote wa siasa
ikiwemo viongozi wa vyama vya siasa vinavyoshiriki katika uchaguzi Mkuu ili
kuona namna bora ya kufanya uchaguzi katika hali ya amani na utulivu.
“Jeshi la Polisi
halitasita kumchukulia hatua za kisheria mgombea, kiongozi, mfuasi au chama
chochote cha siasa kitakachokiuka agizo hili,” alisema.
Hatua hiyo ya jeshi la
Polisi nchini inatokana na baadhi ya wagombea wa nafasi za Urais kufuatana na
kundi kubwa la wanachama, na wapambe wao wakati wa kuchukua fomu za kuomba
kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ofisi za Tume ya Taifa
ya Uchaguzi hivi karibuni na kuhatarisha usalama ikiwemo kufungwa kwa barabara
na kusababisha baadhi ya shughuli za kijamii kusimama.
Zengwe Hilo lishaanza lol!!!! Always is something dam!!!!!
ReplyDeletekutapatapa tu......haitasaidia kitu ni sawa kuzuia mafuriko kwa mkono
ReplyDelete