Meneja Mfuko wa Barabara
Bw.Joseph Haule akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
hivi karibuni alipokuwa akiwasilisha ripoti ya mafanikio ya utekelezaji
wa Mfuko wa Barabara kwa Serikali ya awamu ya nne.
Naibu Meneja Masuala ya
Kiufundi Bw. Ronald Lwakatare kutoka Taasisi ya Mfuko wa Barabara
akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
……………………………
Na Lorietha Laurence-Maelezo
Bodi ya Mfuko wa Barabara
nchini(RFB) imefanikiwa kufanya maboresha ya barabara kwa kiwango cha
lami katika kipindi cha miaka kumi ya uongozi wa Serikali ya awamu ya
nne wa Mhe. Jakaya Kikwete.
Akizungumza na waandishi wa
habari Dar es Salaam Jana Bw. Joseph Haule amesema kuwa matengenezo
hayo yamefanikisha ujenzi wa barabara kuu zinazounganisha mikoa
mbalimbali nchini kukamilika kwa asilimia 89 huku zile za Wilaya na Miji
kwa asilimia 57.
“ kazi kubwa ya Mfuko huu ni
kukusanya mapato kupitia vyanzo mbalimbali ikiwemo tozo za barabarani
na ushuru wa mafuta na baadaye kuzigawa kupitia taasisi zinazohusika
na ujenzi wa barabara ikiwemo TANROADS, Wizara ya Ujenzi na Ofisi ya
Waziri Mkuu “ alisema Bw. Haule
Aidha aliongeza kuwa Mfuko huo
umefanikisha ujenzi wa daraja la Mabatini jijini Mwanza ,daraja la
Mwanhunzi na daraja la Mbutu linalounganisha Igunga na Shinyanga
pamoja na ununuzi wa vivuko kikiwemo kile cha Mv Malagarasi.Mbali na hayo Bw.Haule aliongeza
kuwa Bodi hiyo inaendelea kuhakikisha barabara zinatunzwa kwa
kudhibiti magari ya mizigo yanayozidisha uzito unaochangia uharibifu wa
barabara kwa kuanzisha mfumo wa kisasa wa kamera utakaokuwa
unaratibiwa na mfuko huo.
Mfuko huo umefanikiwa kuanzisha
ujenzi wa barabara kwa kutumia mawe ambao ni wa gharama nafuu na wa
kudumu kwa muda mrefu,hata hivyo miradi hiyo imeanza kutekeleza katika
mikoa ya Kigoma na Mwanza.
Kutokana na mtandao wa barabara
kufanyiwa matengenezo ya mara kwa mara imesaidia kuongeza ubora wa
barabara na kupanua wigo wa biashara kati ya Tanzania na nchi za jirani
ikiwemo Zambia,Malawi,Burundi,Rwanda na Uganda.
Mbali na mafanikio hayo Mfuko
huounakabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa bajeti
kutokana na fedha zinazopatikana kutokukidhi mahitaji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...