Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akiongea na Maafisa
Vijana na kuwataka kutumia elimu na ujuzi walioupata katika mafunzo ya
ujasiriamali na ubunifu katika kuisaidia serikali kutimiza dhamira yake
ya kuwainua vijana kiuchumi, wakati wa hafla ya ufungaji wa mafunzo ya
ujasiriamali na ubunifu kwa Maafisa Vijana jijini Arusha.
Mkurugenzi Mkuu wa Chuo cha
Uongozi cha Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI) Prof Bonard Mwape
akiwaeleza maafisa vijana kuhusu umuhimu wa kubadilisha fikra za vijana
ili kuwawezesha kujiajiri kupitia mafunzo watakayowapatia ya
ujasiriamali, wakati wa hafla ya ufungaji wa mafunzo ya ujasiriamali na
ubunifu kwa Maafisa Vijana jijini Arusha.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akiwakabidhi Baadhi ya
Maafisa Vijana vyeti vya kuhitimu mafunzo ya Ujasiriamali na ubunifu,
wakati wa hafla ya ufungaji wa mafunzo ya ujasiriamali na ubunifu kwa
Maafisa Vijana jijini Arusha.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akimueleza jambo
Mkurugenzi Mkuu wa Chuo cha Uongozi cha Mashariki na Kusini mwa Afrika
(ESAMI) Prof.Bonard Mwape wakati wa hafla ya ufungaji wa mafunzo ya
ujasiriamali na ubunifu kwa Maafisa Vijana jijini Arusha.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga na Mkurugenzi Mkuu wa
Chuo cha Uongozi cha Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI) Prof. Bonard
Mwape wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Vijana na Baadhi ya
watumishi wa Wizara ya Habari na Chuo cha ESAMI.
………………………………………………………………………………………….
Habari Picha na Hassan Silayo-MAELEZO ARUSHA
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kuweka
mipango endelevu ya kuwasaidia vijana ili waweze kujiajiri na kuajiri
wengine.
Hayo yamesemwa leo Jijini Arusha na Katibu Mkuu Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga wakati akifunga
mafunzo ya ujasiriamali na ubunifu yaliyotolewa kwa Maafisa Vijana.Sihaba alisema kuwa kundi la vijana ni kundi kubwa lenye
changamoto nyingi za kiuchumi na kijamii zinazopelekea kupunguza ufanisi
katika uzalishaji mali kuanzia ngazi ya familia na taifa kwa ujumla.
“Serikali inadhamira ya dhati ya kuwawezesha vijana kiuchumi
kupitia miradi mbalimbali ya kimaendeleo ili kuwafanya vijana waweze
kujikimu kimaisha kwa kujiajiri au kuajiri wengine na hii inatokana na
serikali kutambua changamoto zinazowakabili vijana ikiwa ni kundi muhimu
katika jamii” Alisema Sihaba.
Aidha Sihaba aliwataka Maafisa Vijana kutumia elimu na ujuzi
walioupata katika mafunzo hayo katika kuisaidia serikali kutimiza
dhamira yake ya kuwainua vijana kiuchumi na kulifanya kundi hilo
kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji mali kwa manufaa yao
na Taifa kwa ujumla.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Chuo cha Uongozi cha Mashariki na Kusini
mwa Afrika (ESAMI) Prof Bonard Mwape aliishukuru Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo kwa kuwapa nafasi ya kutoa mafunzo hayo kwa
Maafisa Vijana watakayo yatumia katika kuwabadilisha fikra vijana na
kuwafanya waweze kujiajiri kupitia ujasiriamali.
Prof. Mwape aliongeza kuwa huu ni mwanzo wa mambo mazuri
yanayokuja kwa ajili ya vijana na kwa ushirikiano na Serikali kupitia
Wizara watahakikisha vijana wanakuwa wanakuwa sehemu muhimu katika jamii
hasa katika shughuli za uzalishaji mali.
Akizungumzia kuhusu faida za mafunzo hayo Afisa Maendeleo ya
Jamii wa Jiji la Arusha Bi. Hanifa Ramadhani alisema kuwa watatumia
mbinu walizojifunza katika mafunzo hayo ili kukidhi mahitaji ya vijana
na kuwawezesha kujiajiri kupitia ujasiriamali na kuwafanya kushiriki
katika shughuli za uzalishaji mali.
Mafunzo hayo ya Ujasiriamali na Ubunifu yameandaliwa kwa
ushirikiano wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Chuo
cha Uongozi cha Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI) kwa lengo la
kuwawezesha vijana kujiajiri na kuajiri wengine
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...