Kuna upotoshaji wa Makusudi uliozagaa kwenye Mitandao ya Kijamii kuwa Mabasi Yaliyozinduliwa Tarehe 17/08/2015  kuwa.

1. Ati ni ya Kichina

2. Milango ya kushukia na kupandia Abiria Iko kushoto hivyo hayaendani na Miundombinu iliyojengwa.

HUO NI UZUSHI WENYE LENGO LA KUWAPOTOSHA WATANZANI WALIOCHOSHWA NA MSONGAMANO UNAOONGEZEKA SIKU HADI SIKU

TAARIFA SAHIHI KUTOKA KWENYE MAMLAKA HUSIKA HII HAPA:

1. Kiwanda Kilicho Assemble (Kuunganisha) Mabasi haya kinaitwa Golden Dragon cha China.

2. Aina ya Injini  ni CUMMINS  ya Marekani (USA)

3. Aina ya Giaboksi ni    VOITH ya Ujerumani.

4. Mfumo wa Stelingi  ni ZF ya Ujerumani.

5. Mgumo wa Difu ni kutoka Marekani (USA).

6. Aina ya Suspension (Za upepo) Air Suspension kutoka Marekani (USA).

7. Mfumo wa Breki ni WABCO

8. Aina za Mabasi ziko mbili.  Articulated Mita kumi na nane almaarufu (Ikarusi) Kutoka Hungary zitakazopita kwenye barabara Maalumu za zege zilizojengwa na Mabaai ya mita kumi na mbili yanayoitwa (Feeder) Mabasi Mlisho yatakayotumia vituo vilivyoko nje ya mfumo Mfano Kituo cha Shekilango, Moroco Hotel, Mwanamboka na Magomeni Mapipa kuwapeleka na kuwaleta kwenye Mfumo.

9. Milango ya kupanda na kushukia Abiria ipo kulia na kushoto ili kukidhi mahitaji ndani na nje ya mfumo ambayo idadi yake ni Minne kila upande ila itatumika mitatu na mmoja niwa dharula kila upande.

10. Urefu kutoka ardhini kwa milango ya kushoto ya Basi ni Sentimita thelathini (30) ambayo hata mtoto anaweza kushuka bila msaada wa mtu mzima.

11. Urefu wa Milango ya kulia ni Sentimita tisini (90) sawa na urefu wa Platform za kila kituo cha DART unaomuwezesha hata mtu mwenye mahitaji maalum Kuingia na kutoka ndani ya basi bila msaada wa mtu.

12. Ndani ya basi kuna eneo la kukaa watu wenye Mahitaji maalum.
Walemavu, Wazee na Mama wajawazito.

13. Mfumo wa ulipaji nauli unafanyika vituoni kama ilivyo kwenye kivuko pale Kivukoni hivyo basi hili halina Kondokta. Makondakta wapo vituoni.

14. Muda wa Safari kutoka Kivukoni hadi kimara ni wastani wa dakika thelathini (30) ikihusisha muda wa kushusha na kupakia kwenye Vituo vya DART.

15. Ni marufuku kwa chombo ama mwananchi kutumia barabara maalum za Mabasi. Wananchi watumie maeneo yaliyotengwa maalum kulingana na mahitaji. Watumiaji wa Bodaboda wanatakiwa kupita kwenye barabara zinazotumiwa na magari ya Kawaida na siyo eneo lililotengwa kwa ajili ya Watembea kwa Miguu.

HIZI NDIZO TAARIFA MUBIMU NA RASMI KWA WATANZANIA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Ahsante kwa taarifa!

    ReplyDelete
  2. I miss old good day kila habari ilikuwa ya kweli

    ReplyDelete
  3. Tatizo DART BRT mradi wenu umekaa kisiri sana mnawapasha habari watendaji wakuu/wakubwa lakini watumiaji hasa wa usafiri huo hamuwashirikishi kwa karibu na hivyo kukaribisha habari za uvumi.

    Kitengo cha DART BRT lazima kiwe pro-active kwa kutoa habari sahihi kwa wakati muafaka na pia elimu ya matumizi ya mabasi hayo na wadau wengine wanaotumia barabara zilizo sambamba na za DART-BRT.

    Muhimu ikiwemo labda kuweka sheria ndogo ndogo kuwa magari mengine yakitumia njia hiyo maalum ya mabasi ya mwendo kasi basi watapigwa faini na kufikishwa mahakamani ikiwemo uwezekano wa kunyanganya leseni za udereva kwa wanaokiuka utaratibu.

    Maana bila taratibu na elimu basi mradi huo wa gharama kubwa unaweza kushindwa kufikia malengo yake kama safari ya Kimara -Mjini badala ya kuwa dakika 30 ikawa dakika 60 mpaka 90.

    Mdau
    Sheria kwa shuruti

    ReplyDelete
  4. Asantenii sana kwa ufafanuzi du ndugu zangu Ukawa ikulu sio sehemu ya kufosi hata kwa njia za uongo #hapa kazi tu #teammagufuli

    ReplyDelete
  5. santeee.......watu hawakosi nenoo...wanaozusha waulize yao mazuri yako wapi

    ReplyDelete
  6. Bidhaa za China ziko kila mahali siku hizi, la muhimu ni kuwa na usafiri mzuri jijini.

    Siku za nyuma jiji hili lilikuwa na mabasi mengi ya UDA kutoka Hungary ikiwemo IKARUS ndogo na kubwa zilizokuwa zikiitwa IKARUS rafiki yangu wa nchi jirani alikuwa akiniambia tulipokuwa tukija Dar tukiona jinsi mabasi yalivyokuwa yakitoa huduma tulikuwa tunawaona mko mbali. Maikarus makubwa yalikuwa yanabeba sana abiria.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...