WANANCHI wa vijiji vya Ilole, kitumbuka, Ilambilole, Ikengeza, Chamdindi na vingine vilivyopo Katika wilaya ya Kilolo na Ismani mkoani Iringa wailalamikia serikali kwa kushindwa kutatua kero ya maji iliyodumu kwa muda mrefu Katika maeneo hayo.
Wakizungumza kwa huzuni mbele ya mkuu wa mkoa wa Iringa aliyefanya ziara ya kugagua miradi ya maji Katika wilaya hizo Mh Amina Masenza wananchi hao walisema kumekuwa na ubabaishaji wa kisiasa juu ya namna ya kupelekewa maji jambo ambalo linawafanya waweze kutumia maji yasiyo salama kwa afya zao.
Wananchi hao walisema kumekuwa na miradi ya maji mingi ambayo ilitajiwa kuwanzishwa Katika wilaya zao lakini mpaka sasa hakuna utekerezaji wowote juu ya kutatua kero hizo pamoja na kuwa na vyanzo vizuri vya maji.
“mh mkuu wa mkoa tumeahidiwa sana juu ya kuletewa maji safi huku vijijini matokeo yake hakuna lililofanyika tumekuwa watu wa kudanganywa kabisa hata tukiangalia umbali wakilipo chanzo cha maji hata wangesema tuchimbe mitalo wenyewe tungechimba ila wanatudanganya na siasa zao hatuyajui maji ya baridi toka tunazaliwa tunatumia maji ya chumvi tuoneeni huruma jamani” walisema wananchi.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...