Na Jenikisa Ndile-MAELEZO 
Serikali ya Tanzania na Ujerumani zimetiliana saini mikataba miwili ya misaada yenye thamani ya jumla ya Euro milioni 17 ambazo ni sawa na Tsh. Bilioni 39.1 kusaidia sekta ya afya, maji na maliasili. 
 Makubaliano hayo yamesainiwa jijini Dar es salaam kati ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Egon Kochanke ili kuleta mafanikio na maendeleo katika. 
 Aidha, Dkt. Likwelile amemhakikishia Balozi Kochanke na ujumbe wake kuwa msaada walioipa Serikali utatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuleta ufanisi na kuongeza nafasi za ajira na hatimaye kuchangia katika kuboresha uchumi nchini. 
Kwa upande wake Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Egon Kochanke amesema kuwa serikali ya Ujerumani itaendelea kushirikiana na Tanzania kwa kuzingatia uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi hizo mbili. 
Zaidi ya hayo, serikali hizo mbili zimesaini mkataba wenye thamani ya Euro milioni 10 ambazo ni sawa na Tsh bilioni 23 kuisaidia usimamizi wa hifadhi ya Taifa ya ya wanyama mwitu ya Selous
 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (wa kwanza kulia) akisaini hati ya makubaliano katika hafla ya utiaji saini wa mikataba 2 ya sekta za maji, afya na maliasili Alhamisi Agosti 13, 2015 Jijini Dar Es Salaam. Wa pili kulia ni Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Egon Kochanke.
 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kulia) akibadilishana hati ya makubaliano na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Egon Kochanke (kushoto) katika hafla ya utiaji saini wa mikataba 2 ya sekta za maji, afya na maliasili

 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile akiongea na baadhi ya viongozi wa Wizara hiyo, ujumbe wa ulioandamana na Balozi wa Ujerumani pamoja na waandishi wa habari mara baada ya utiaji saini wa mikataba 2 ya sekta za maji, afya na maliasili 
 Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Egon Kochanke akiongea na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Fedha, wajumbe kutoka Ujerumani pamoja na waandishi wa habari mara baada ya utiaji saini wa mikataba 2 ya sekta za maji, afya na maliasili 
Viongozi kutoka Wizara ya Fedha, wajumbe kutoka Ujerumani pamoja na waandishi wa habari waliohudhuria hafla ya utiaji saini wa mikataba 2 ya sekta za maji, afya na maliasili  Alhamisi Agosti 13, 2015 Jijini Dar Es Salaam. 
Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...