New Picture (13)
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake akikagua mradi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na Shirika hilo eneo la Napupa Mjini Masasi.
New Picture (14)
Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Bw. Paul Mkami(kushoto) akimuonyesha Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake ramani ya eneo la ardhi lililopewa NHC kwa ajili ya kujenga nyumba za gharama nafuu Wilayani humo.
New Picture (15)
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake wakitembelea eneo la kujenga nyumba za gharama nafuu Wilayani Namtumbo alipofanya ziara yake katika Mkoa wa Ruvuma.
New Picture (16)
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake wakikagua hatua zilizofikiwa katika ujenzi wa Ofisi ya Shirika Mkoani Ruvuma ambapo ameagiza Ofisi hiyo iwe imekamilika ndani ya mwezi mmoja ili kuwapa fursa wateja na wananchi kupata huduma kwa urahisi. Kwa muda mrefu NHC haikuwa na Ofisi ya kudumu katika Mkoa wa Ruvuma kutokana na sguli za Mkoa huo kusimamiwa na Mkoa wa NHC wa Iringa.
New Picture (17)
Mradi wa nyumba za gharama nafuu unaojengwa na NHC Wilayani Makete nao ulipata fursa ya kutembelewa na Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake. Hapa Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Mikoa Bw. Raymond Mndolwa anaonyesha eneo ambalo litajengwa Kituo cha biashara ili kuhudumia wakazi watakaoishi katika nyumba hizo za kisasa zinazouzwa kwa wananchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...