
JESHI
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam linatarajia kuzindua mashindano ya michezo mbalimbali kwa lengo la kuwashirikisha wananchi wa
rika zote na itikadi
mbalimbali
yatakayojulikana“KAMISHNA
KOVA CUP”.
Madhumini ya mashindano haya ni ni Kuwaunganisha wananchi wenye itikadi
mbalimbali ili kupitia mashindano
haya watakaoshiriki watajifunza
masuala ya usalama, uzalendo na kuzingatia utaifa kwa madhumuni ya kuwashirikisha
kikamilifu katika ulinzi wa nchi na kudumisha amani na
utulivu katika jiji
la Dar es
Salaam na mikoa mingine.
Lengo lingine ni Kuishirikisha jamii kuondokana na dhana ya kutenda uhalifu wa
aina mbalimbali kama vile ujambazi, matumizi ya aina mbalimbali ya madawa ya kulevya, wizi katika mitandao,uzururaji, na kukaa
katika vijiwe bila kazi.
Pia Kupitia michezo mbalimbali, jamii itafaidika
kupata elimu juu ya umuhimu wa jukumu la msingi la kushiriki katika ulinzi na usalama wa
nchi hii, itakuwa ni fursa
nzuri kujua madhara ya
kujihusisha na vitendo vya uhalifu.
Katika michezo watajifunza kujenga au kuimarisha
mahusiano mema baina ya Jeshi la Polisi na
jamii kwa ujumla
kupitia dhana ya
Polisi Jamii itatekelezwa kwa
vitendo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...