Na Frank Shija, WHVUM

Vijana watakiwa kujitokeza katika maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani ambayo kitaifa yatafanyika tarehe 12 Agosti jijini Dar es Salaam huku kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni “Ushiriki wa Vijana katika masuala ya Kiraia”

Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam.

Bibi Sihaba amesema kuwa maadhimisho hayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka ikiwa ni kutambua mchango wa Vijana katika kuleta maendeleo ya taifa na jamii kwa ujumla kwa kuwa ndiyo kundi kubwa la nguvu kazi yenye kuleta chachu ya maendeleo kupitia ubunifu.

“Natoa wito kwa vijana wote nchini kushiriki katika kuadhimisha Siku hii muhimu kwa kujihusisha na shughuli mbalimbali za kijamii katika maeneo yao, kwa wale wa Dar es Salaam ni vyema wakajitokeza na kushiriki maadhimishio hayo ambayo kitaifa yanafanyika mkoani hapa” Alisema Sihaba.

Aidha Katibu Mkuu huyo aliongeza kuwayatafikia kilele siku ya Jumatano ya tarehe 12 Agosti yatatanguliwa na Kongamano litakalofanyika mnamo tarehe 10 mwezi huu katika ukumbi wa Karimjee nakushirikisha zaidi ya Vijana 150 watakao jadiliana mada mbalimbali ikiwemo ushiriki wa vijana katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Aliongeza kuwa sambamba na maadhimisho hayo siku ya kilele kutakuwa vijana watapata fursa ya kutoa na kupata burudani mbalimbali kupitia matamasha na michezo, pia siku nhiyo itatumika kwa vijana kuonyesha kazi zao zikiwemo za ubunifu.

Katika kuhakikisha maadhimisho hayo yanafanyikiwa Serikali imekuwa ikishirikiana na wadau mbalimbali katika mikakati na uendelezaji wa Vijana nchini amjbapo baadhi ya wadau hao ni pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), AMREF,ILO, PSI, IYF, Restless Development na wadau wote ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa wakijihusisha na vijana.

Siku ya Kimataifa ya Vijana ilianza tangu mwaka 1991 nchini Australia ikiwa na lengo la jumuiya ya Kimataifa na jamii kwa ujumla kupata fursa ya kusherehekea na kutambua nafasi ya Vijana katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika nchi zao, na mwaka 1998 ilikubaliwa na jopo Mawaziri wanaoshughulikia Vijana na hatimaye Umoja wa Mataifa uliridhia rasmi kuitambua siku hiyo kuwa ya maadhimisho Kimataifa ambapo mwaka 2000 nchi wanachama wa Baraza la Umoja wa Mataifa ikiwemo Tanzania walianza kuadhimsha siku hiyo muhimu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga akifurahia jambo na waandishi wa habari wa wa Kituo cha Redio cha TBC Taifa walipomtembelea ofisini kwake jana.Waliosimama kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana wa wizara hiyo Bw. James Kajugusi na wa mwisho kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bibi. Concilia Niyibitanga.Waandishi hao walifika ofisini kwa Katibu Mkuu huyo kwaajili ya mahojiano maalum kuhusu maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani ambayo kitaifa inaadhimishwa tarehe 12 Agosti jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga akifanya mahojiano maalum kuhusu maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani na mwandishi wa habari kutoka Redio ya Taifa TBC Taifa Bibi. Betty Tesha. Maadhimisho hayo kitaifa yanaadhimishwa tarehe 12 Agosti jijini Dar es Salaam. Picha na Frank Shija, WHVUM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ujana Mwisho umri gani?

    ReplyDelete
  2. Ujana unaanza miaka 18 na MWISHO wake miaka 46 tu.Ukianza 47 basi wewe kingwangwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...