Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupunguza Matatizo ya Mapafu Duniani iliyopo nchini Tanzania (WLF), Dk. Nguke Mwakatundu akifungua semina hiyo leo jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupunguza Matatizo ya Mapafu Duniani iliyopo nchini Tanzania (WLF), Dk. Nguke Mwakatundu akifungua semina hiyo leo jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa Huduma za Kliniki wa Taasisi ya Kupunguza Matatizo ya Mapafu Duniani iliyopo nchini Tanzania (WLF), Dk. Sunday Dominico akiwasilisha mada katika semina hiyo leo ofisi za WLF. Mkurugenzi wa Huduma za Kliniki wa Taasisi ya Kupunguza Matatizo ya Mapafu Duniani iliyopo nchini Tanzania (WLF), Dk. Sunday Dominico akiwasilisha mada katika semina hiyo leo ofisi za WLF,Mikochini Jijini Dar.Meneja Mawasiliano wa Taasisi ya Kupunguza Matatizo ya Mapafu Duniani iliyopo nchini Tanzania (WLF), Victoria Marijani.Meneja Mawasiliano wa Taasisi ya Kupunguza Matatizo ya Mapafu Duniani iliyopo nchini Tanzania (WLF), Victoria Marijani,akifafanua jambo.Waandishi wa Mitandao ya Kijamii Wapewa Elimu ya Afya na UzaziMeneja Mawasiliano wa Taasisi ya Kupunguza Matatizo ya Mapafu Duniani iliyopo nchini Tanzania (WLF), Victoria Marijani.Meneja Mawasiliano wa Taasisi ya Kupunguza Matatizo ya Mapafu Duniani iliyopo nchini Tanzania (WLF), Victoria Marijani.

BAADHI ya wanahabari wa mitandao ya jamii jijini Dar es Salaam wamepewa mafunzo juu ya taarifa za uzazi na afya ya mama na mtoto ili waweze kuelimisha zaidi jamii kupitia mitandao yao dhidi ya taarifa hizo. 

Akizungumza wakati akifungua semina hiyo, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupunguza Matatizo ya Mapafu Duniani iliyopo nchini Tanzania (WLF), Dk. Nguke Mwakatundu alisema taasisi yake imeamua kutoa mafunzo hayo kwa  wanahabari hao ili waweze kuwa mabalozi wazuri wa kuelimisha jamii kupitia mitandao yao juu ya umuhimu wa kupambana na vifo vya mama na  mtoto vinavyoendelea kutokea kila uchao.

 Alisema kazi ya kupunguza vifo vya mama na mtoto si jukumu la madaktari au hospitali pekee lakini jukumu la jamii nzima kukabiliana na huduma hiyo, alisema vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya jamii inakilasababu za kuonesha mapungufu na kueleza changamoto katika huduma za afya zinazotolewa kwa lengo la kuboresha zaidi huduma hizo.

 Alisema tatizo la elimu ya afya ya uzazi ni kubwa nchini kwani takwimu zinaonesha kwa kila saa moja kuna mama anayepoteza maisha kutokana na  matatizo ya uzaziSerikali. "...Kila siku kuna akinamama takribani 24 wanapoteza maisha kutokana na matatizo ya uzazi nchini," alisema Dk. Mwakatundu. 

Awali akizungumzia hali halisi ya uzazi wa mpango nchi, Meneja Mawasiliano wa WLF, Victoria Marijani alisema kuna faida kuwa ya kuzingatia Uzazi wa Mpango kwani ni uwekezaji wenye faida na endelevu ambao unachangia kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa kiasi kikubwa hadi asilimia 44. 

Aliongeza kuwa uwekezaji huo wa ziada katika afya, elimu, usawa wa kijinsia na uwepo wa sera wezeshi za kiuchumi vitaiwezesha nchi kupata manufaa yatokanayo na ukuaji wa haraka wa uchumi. Alisema familia zinazotumia uzazi wa mpango zinakuwa na uwezo wa kuwatimizia watoto mahitaji yao muhimu kama chakula, elimu, mavazi, huduma za afya na makazi. 

"...Atapata muda wa kushiriki katika shughuli za jamii, Atamudu kujiwekea akiba, Atakuwa na amani na upendo kwa familia yake. Alisema kiwango kikubwa cha vifo vya watoto chini ya miaka 5 (vifo 81 kwa vizazi hai 1000) Kiwango kidogo cha utumiaji wa njia za kisasa za uzazi wa mpango (Asilimia 27). Wastani wa utumiaji wa njia za kisasa za uzazi wa mpango hapa nchini bado ni mdogo. Ni asilimia 27 tu ya wanawake walio kwenye umri wa kuzaa ndio wanaotumia njia za kisasa za Uzazi wa Mpango. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...