Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumaza na vijana wakati wa
maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani iliyoadhimishwa katika Viwanja
vya Mnazi Mmoja jana jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika
la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Bibi.
Natalia Kanem.
Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani
(UNFPA) Bibi. Natalia Kanem (kulia) akisalimiana na mmoja wa vijana waliokua
katika banda la familia wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana
duniani iliyoadhimishwa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jana jijini Dar es
Salaam.
Naibu Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel
(mwenye miwani katikati) katika picha ya pamoja na vijana walioshiriki
maadhimisho ya siku kimataifa ya vijana duniani jana katika Viwanja ya Mnazi
Mmoja.
Baadhi ya vijana wakiandamana kuelekea katika Viwanja vya Mnazi Mnoja kuadhimisha siku ya kimataifa ya vijana duniani, kushoto mwenye tisheti ya bluu ni Mkurugenzi Msaidizi Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Venerosa Mtenga. Siku hiyo imeadhimishwa jana katika viwanja hivyo.Picha
na: Genofeva Matemu – Maelezo
Na: Genofeva
Matemu – Maelezo
Tarehe:
13/08/2015.
Vijana nchini
wametakiwa kuwajibika kutafuta taarifa sahihi kutoka katika vyanzo sahihi na
kuzingatia utoaji wa taarifa zilizo sahihi haswa katika kipindi hiki
tunapoelekea katika uchaguzi mkuu.
Rai hiyo
imetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Prof. Elisante Ole Gabriel wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani jana katika Viwanja vya Mnazi
Mmoja Jijini Dar es Salaam.Prof. Gabriel
aliwataka vijana kuachana na taarifa za uchochezi zinazosambazwa katika
mitandao mbalimbali zisizokua na ukweli ndani yake na kuzishikilia kwa
kuhamasisha vijana wenzao kuamini mambo yasiyokua sahihi.
“Vijana wana
haki ya kupata taarifa sahihi, haki ya kupiga kura na kumchagua kiongozi mwenye
maslahi katika nchi, na kuheshimu sheria zilizopo kwa kuwa na maadili mema
yatakayowawezesha kujengewa heshima na kuthaminiwa katika jamii” alisema prof.
Gabriel.
Akizungumza
wakati wa maadhimisho hayo Mwakilishi Mkazi kutoka shirika la umoja wa mataifa
linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Bibi. Natalia Kanema aliitaka
jamii kuhakikisha kuwa vijana wanashirikishwa kutoa maamuzi katika masuala ya
kifamilia, kijamii na kitaifa.
Bibi. Kanema
amesema kuwa vijana ni taifa la kesho, wanapaswa kushikilia ndoto zao na
kujiongeza hivyo jamii iwakumbatie na kuwashirikisha katika maamuzi kuweza
kujenga taifa lililokomaa na lenye weledi wa hali ya juu.
Aidha kijana
Hesein Melele kutoka asasi ya vijana chini ya umoja wa mataifa (YUNA) amewataka
vijana nchini kuondokana na dhana ya kulalamikia Serikali bali wajitokeze
kushiriki katika masuala mbalimbali na kuachana na tabia ya kusubiri
kushirikishwa.
Bw. Melele
aliwahasa vijana kutumia haki yao ya kikatiba kushiriki katika uchaguzi kwa
amani na utulivu ili kuweza kuchagua kiongozi mwenye maslahi katika jamii
atakayeongoza nchi kwa amani.
Naye
mwanafunzi kutoka shule ya Sekondari Jangwani Bi.Tatu Ahmed amewataka vijana
wenzake nchini kuwa na maadili mema katika jamii na kutumia fursa mbalimbali
walizonazo kujikwamua kiuchumi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...