Viongozi waandamizi wa
Tanzania Bloggers Network (TBN) wakigonganisha glasi na Afisa Mahusiano ya Umma
wa Ubalozi wa Marekani Bi. Marissa Maurer (wa tatu kushoto) na Afisa wa Siasa na Uchumi wa
ubalozi huo Bw. Vincent Spera (wa pili kushoto) walipokutana jijini Dar es salaam kwa mazungumzo yasiyo rasmi ili kubadilishana mawazo ya
njia bora ya kuendeleza tasnia hiyo ya habari za mtandao inayokuja juu kwa kasi
nchini.
TBN ni umoja wa bloggers wapatao 100 waliouunda ili kujiendeleza na
kusimamia maslahi yao huku wakisaidia kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya
Taifa nay a tasnia ya habari kwa jumla. Wengine toka kulia ni wajumbe wa TBN Max Mello, Joachim Mushi (Mwenyekiti), Monica Mara (Afisa Mipango), Hadija Kalili (Katibu), Shamim Mwasha (mtunza hazina) na Afisa habari wa ubalozi huo Japhet Sanga. Picha kwa hisani ya TBN
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...