Na Geofrey Tengeneza 
Waandishi wa habari sita kutoka vyombo vya habari mbalimbali kutoka Tanzania wako ziarani chini Estonia kwa mwaliko wa Serikali ya nchi hiyo. 
 Lengo la ziara hiyo ni kutoa fursa kwa wandishi wa habari wa Tanzania kujifunza na kujionea shughuli mbali mbali katika sekta za teknolojia ya mawasiliano , elimu, utalii, afya n.k. ili kuandikia habari hizo n chini Tanzania. 
Katika siku mbili za mwanzo za ziara hiyo ya siku tano, waandishi hao kutoka Tanzania tayari wametembelea sehemu kadhaa ikiwa ni pamoja na kampuni kubwa inayoongoza katika teknolojia ya mawasiliano chini Estonia iitwayo Nortal, kituo cha tiba maalumu ya matope na chumvi kilichopo katika mji wa Haapsalu na kuzungumza na Meya wa mji huo wa Staili Mstahiki Meya Maret Sukles. Katika ziara hiyo inayoratibiwa a na Chuo Kikuu cha Tullinn shule kuu ya Media and filming ya Balticts, waandishi hao wamefuatana  na afisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Sweden Bw. Jacob Msekwa.
 Waandishi wa habari kutoka Tanzania katika picha na mwakili shi wa kampuni ya teknolojia ya mawasiliano ya Nortal muda mfupi baada ya kutembelea kampuni hiyo jijini Tallinn Estonia leo.
Meya wa mji wa Haapsalu katika picha ya pamoja na baadhi ya waandishi wa habari wa Tanzania baada ya mazungumza na wandiishi hao leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...