Mratibu wa Taifa wa Mpango wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dkt. Upendo Mwingira, akielezea majukumu ya mpango huo wakati wa uzinduzi wa kambi ya kuwafanyia upasuaji watu wenye tatizo la ugonjwa wa mabusha Manispaa na Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara,iliyofanyika katika hospitali ya Mkoa ya Ligula.
Kaimu Mkuu wa Wilaya akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kambi ya kuwafanyia upasuaji watu wenye ugonjwa wa mabusha.
Dkt. Upendo Mwingira akiwafariji wagonjwa waliokwishafanyiwa upasuaji wa mabusha katika hospitali ya mkoa ya Ligula.Upasuaji huo ni wa siku 5. Mkoa wa Mtwara una takribani watu wapatao 2,500 wanaosumbuliwa na ugonjwa wa mabusha.Kambi hii itafanyika kwa watu waliojiandikisha na itatolewa bila ya malipo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...