Na Freddy Macha
Baada ya mwezi mzima wa kelele, vifijo na chereko- chereko, hatimaye siku mahsusi ya burudani na biashara itawadia kesho Jumamosi 29 Agosti, 2015. Huu ni wakati wanariadha wa Kenya wanaongoza "meza ya medali " mashindano yanayoendelea mjini Beijing, China.
Tamasha maalum la “Kenya in the Park” linaloongozwa na kikundi cha ngoma cha Malaika Dance na Taifa Radio FM chini ya msanii na mwanahabari, Lydia Olet, mkazi London, yatafanyika uwanja wa mpira wa Rugby na Soka kitongoji cha West Ham, London ya mashariki. Shughuli hii itakayoanza saa tano asubuhi hadi mbili usiku ni bure na kwa wananchi, wapenzi na marafiki wote wa Kenya. Fahari ya Afrika Mashariki.
Habari zaidi pitia www.kenyainthepark.com

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...