Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali

Iddi akikabidhiwa Fomu za kuwania nafasi ya Ujumbe wa Baraza la
Wawakilishi Zanzibar Jimbo la Mahonda kutoka kwa Afisa wa Uchaguzi
Wilaya ya Kaskazini B Ndugu Makame Pandu Khamis.

 Afisa wa Uchaguzi Wilaya ya Kaskazini B Nd. Makame

Pandu Khamis akitoa maelezo kumpatia Balozi Seif ya namna ya ujazaji
wa fomu za kuwania Uwakilishi Jimbo la Mahonda Ofisini kwake Mahonda
Wilaya ya Kaskazini “B” Mkoa wa Kaskazini Unaguja.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
akisalimiana na baadhi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi mara baadaya kuchukuwa fomu za kuwania Uwakilishi Jimbo la Mahonda hapo Ofisi yaTume ya Uchaguzi Wilaya ya Kaskazini B iliyopo Mahonda.

WANACHAMA mbali mbali wa Vyama vya Siasa Nchini walioomba na
kuthibitishwa na vyama vyao kuwania nafasi mbali mbali za uongozi
wameanza rasmi kujitokeza kuchukuwa fomu za kuwania kugombea nafasi
walizoomba katika  Ofisi za Tume ya Uchaguzi za Wilaya.

Zoezi hilo litalowashirikisha wagombea nafasi za Ubunge, Uwakilishi na
Udiwani linatarajiwa kuendelea hadi Tarehe 6 Septemba 2015 ambapo
wanaochukuwa fomu hizo watalazimika kujaza vipengele vyote vinne
vilivyomo kwenye Fomu hizo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikuwa
miongoni mwa wanachama kadhaa wa Chama cha Mapinduzi waliojitokeza
kuchukuwa Fomu hizo ambapo yeye ameamuwa kugombea nafasi ya Ujumbe wa
Baraza la Wawakilishgi Jimbo la Mahonda.
Balozi Seif alikabidhiwa fomu hizo mapema asubuhi na Afisa wa Tume ya
Uchaguzi Zanzibar {ZEC } Wilaya ya Kaskazini “B” Ndugu Makame Pandu
Khamis hapo ilipo ofisi hiyo Mahonda Wilaya ya Kaskazini “B” Mkoa wa
Kaskazini Unguja.

Akikabidhi fomu hizo Afisa huyo wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Wilaya ya
Kaskazini B Ndugu Makame Pandu Khamis amethibitisha kwamba Balozi Seif
Ali Iddi ni Mgombea  halali wa kuwania nafasi ya Ujumbe wa Baraza la
Wawakilishi Jimbo la Mahonda kupitia CCM.

Nd. Makame alisema kwamba uhalali huo unatokana na Ofisi yake kupokea
barua rasmi kutoka Chama cha Mapinduzi { CCM } iliyoainisha na
kuthibitisha kwamba Balozi Seif Ali Iddi ameteuliwa na chama hicho
kuwania nafasi hiyo ya Uwakilishi kwenye Jimbo la Mahonda.

Afisa Uchaguzi huyo wa Wilaya ya Kakaskazini B alifafanua na kuwataka
wagombea wote watakaochukuwa fomu za kuwania nafasi hizo kutumia fursa 
ya kufika kwenye Ofisi hiyo kwa kupata ushauri zaidi wa namna ya
kujaza vyema fomu hizo licha ya kupatiwa maelezo ya awali wakati
wanapokabidhiwa.

Alisema hatua hiyo kwa kiasi kikubwa itatoa fursa pana ya kutatua
changamoyo zinazoweza kujitokeza  na  kuepukwa mapema ili kukidhi
matarahio yaliyopangwa na tume hiyo.

Balozi Seif Ali Iddi alikuwa Mbunge wa Jimbo la Kitope kupitia chama
cha Mapinduzi kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita ambapo kutokana na
mabadiliko yaliyofanywa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar  jimbo hilo

limevunjwa na kuzaliwa majimbo mawili ya Mahonda na Kiwengwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...