Waziri
wa Fedha Saada Mkuya Salum, (kushoto), akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani
ya shilingi milioni moja, mwanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Sara Haule
ikiwa ni malipo ya fao la uzazi wakatinwa uzinduzi wa bodi mpya ya PPF, sambamba
na uzinduzi wa fao hilo la uzazi, Jumanne Agosti 25, 2015.
Waziri Saada Mkuya Salum akitoa hotuba ya uzinduzi
Mkurugenzi
Mkuu wa PPF, William Erio, akitoa hotuba ya ukaribisho na utambulisho nwakati
wa uzinduzi wa bodi mpya ya Mfuko, sambamba na uzinduzi wa Fao la Uzazi, ambapo
wanachama wawili wa Mfuko, Sara Haule na Caroline Kiswaga, walilipwa shilingi
milioni 1 kila mmoja kama malipo ya fao hilo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhan Kijjah, akitoa hotuba yake
Waziri
Saada Mkuya Salum, Mwenyekiti wa Bodi ya PPF, Ramadhan Kijjah, na Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko huo, William Erio, wakiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa
bodi ya PPF
Sehemu ya Wakurugenzi wa Idara mbalimbali za PPF, na Mamenejawaliohudhuria hafla hiyo,
Mratibu wa Kanda za Mfuko wa Pensheni wa PPF,
Mbaruku, akielezea namna fao hilo lilivyozingatia Mwanachama na Mwenza wake
Baadhi ya wajumbe wa bodi ya wadhamini ya PPF
Waziri Saada Mkuya akimpongeza Mwanachama wa PPF, Caroline Kiswaga, baada ya kumkabidhi shilingi milioni moja ikiwa ni malipo ya fao la uzazi
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhan Kijjah, (kushoto),
akimkabidi kadi mpya ya uanachama wa Mfuko nhuo, Waziri wa Fedha, Saada Mkuya
SDalum, wakati wa uzinduzi wa bodi na fao la uzazi, hafla iliyofanyika makao
makuu ya PPF jijini Dar es Salaam, Agosti 25, 2015.
Waziri Saada Mkuya, (kulia), akiagana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PPF,
Waziri Mkuya akiteta jambo na Erio wakati wa hafla hiyo
Meneja
Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Elihuruma
Ngowi, (kulia), akifurahia jambo wakati waziri wa fedha Saada Mkuya Salum,
(kushoto), akimtania Mwanachama wa PPF, Sara Haule, baada ya kupatiwa malipo ya
shilingi milioni moja kama fao la uzazi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...