Na Dixon Busagaga,Moshi.

KAMATI ya Mashindano ya Kombe la jimbo la Vunjo maarufu kama Mbatia Cup 2015 imetenga zaidi ya kiasi cha sh Mil 6 kama zawadi kwa washindi wa mashindano hayo yanayoingia hatua ya nusu fainali pili leo.

Zawadi zilizotengwa ni pamoja na sh Mil 2,Kombe kubwa,Medali za Dhahabu na mipira mitatu kwa mshindi wa kwanza,Sh Mil 1,Kombe la kati,Medali za fedha na Mipira miwili kwa mshindi wa Pili huku mshindi wa tatu akipata Sh 500,000,Ngao,Medali za Shaba na Mpira mmoja.

Mwenyekiti wa kamati hiyo,Danielson Shayo alisema mbali na zawadi hizo kwa washindi,kamati pia imepanga kutoa zawadi za Jezi kwa timu nane ambazo zitafanikiwa kuigia hatua ya nane bora.

“Mshindi wan ne pia tumemuandalia zawadi ya Mpira ,mbali na jezi ambazo itakuwa imepata wakati wa kufanikiwa kuingia hatua ya Nane bora,lakini pia kuna zawadi kwa Mchezaji bora,Mfungaji bora,mlinda mlango bora,timu yenye nidhamu na kocha bora”alisema Shayo.

Shayo alisema mashindano hayo yatakayotumia viwanja vitano vya Chuo cha Ualimu,Marangu,Njia Panda,Kahe Magharibi ,Himo Polisi na Ifati yamepangwa kuchezwa kwa mtindo wa mtoano .
Baadhi ya viongozi wa Chama cha NCCR-Mageuzi jimbo la Vunjo akiwa katika hafla fupi ya kutangaza zawadi kwa washindi wa mashindano ya Mbatia Cup 2015.
Mmoja wa Waratibu wa Mashindano ya Mbatia Cup 2015 yanayofanyika katika jimbo la Vunjo,Danielson Shayo akizungumza wakati wa kutangaza zawadi kwa washindi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...