NAIBU waziri wa maji Amos Makalla leo ametembelea mradi unaotekelezwa kwa ushirikiano wa serikali na mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM) wa uboreshaji huduma ya maji kwa mji wa Geita, Mradi huu unagharimu fedha sh 10 bilioni ambao kukamilika kwake kutaongeza huduma ya upatikanaji maji kutoka asilimia 13 iliopo sasa hadi kufikia asilimia 57.
Kwa mujibu wa tathmini ya kazi iliyofanyika mradi huu unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi august mwaka huu na naibu waziri wa maji ameagiza wahakikishe wananchi wanapata maji wiki ya kwanza mwezi ya mwezi septemba na si vinginevyo.
NAIBU waziri wa maji,Amos Makalla akikagua kazi za uchimbaji mitaro, ulazaji wa mabomba na ukaguzi wa tanki leo katika mji wa Geita
NAIBU waziri wa maji Amos Makalla akitembele maeneo mbalimbali yaliyo na mabomba ya maji.
Mkuu wa mkoa wa Geita Fatma Mwasa akimpokea naibu waziri maji Amos Makalla.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...