Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akizungumza siku ya Jumanne, wakati Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipopitisha Azimio linalowasilisha kwa Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali Malengo na Ajenda mpya za Maendeleo Endelevu ( Ajenda 2030) Anaonekana pia Rais wa Baraza Kuu la 69, Bw. Sam Kutessa .
Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, akiwa na Afisa Mkuu Siongelael Shilla wakati wa upitishaji wa Azimio namba A/69/L.85 kuhusu Ajenda 2030 ambapo baada ya kupitishwa kwa kauli moja azimio hilo wazungumzaji wanaowakilisha makundi ya kikanda walipata fursa ya kuelezea misimamo yao juu ya baadhi ya mambo ambayo walikuwa wakitofautiana kimtizamo na kimsimamo.
Na Mwandishi
Maalum, New York
AFRIKA, imesisitiza
na kubainisha kwamba itatekeleza
malengo mapya ya maendeleo endelevu kwa
kuzingatia maslahi, vipaumbele,
sera, mila na tamaduni ambazo nchi za Afrika zimejiwekea.
Aidha
Afrika inasema kuwa, utekelezaji wa malengo hayo pia utazingatia sheria za kimataifa na ambazo nchi za Afrika
zimeridhia na si vinginevyo.
Hayo yameelezwa na Balozi Fode Seek, Mwakilishi wa Kudumu wa Senegal katika Umoja wa Mataifa ambaye ni Mwenyekiti wa nchi za Afrika kwa mwezi Septemba.
Alikuwa
akizungumza kwa niaba ya nchi
za Afrika wakati Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipokutana siku ya jumanne, kupitisha Azimio namba
A/69/L.85 ambalo linawasilisha ajenda ya
Maendeleo Endelevu (ajenda 2030) itakayotekelezwa kwa miaka 15 ijayo.
Ajenda
2030 inachukua nafasi ya Malengo ya Maendeleo
ya Millenia ( MDGs) yanayofikia ukingoni mwishoni mwa mwaka huu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...