Aliyekuwa mwenyekiti wa IPC Daud Mwangosi (kushoto) akihojiwa na mzee wa matukio daima Bw Francis Godwin ambaye alikuwa ni katibu msaidizi wa IPC juu ya wanahabari kudumisha umoja na mshikamano wakati wa uhai wake.
Mwandishi wa habari wa Chanel Ten mkoa wa Iringa na Mwenyekiti wa cha chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Daud Mwangosi tarehe Kama ya leo miaka mitatu iliyopita aliuwawa katika vurugu za Polisi na wafuasi wa Chadema katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa .
Mwanahabari huyo Daud Mwangosi aliuwawa majira ya saa 10 jioni katika ofisi za Chadema Nyololo huku askari mmoja akijeruhiwa vibaya kwa risasi .
Kabla ya kuuwawa kwa mwanahabari huyo mabomu yaliweza kupigwa eneo hilo kuwatawanya wafuasi hao wa Chadema ambao walikuwa wakigoma kutawanyika eneo hilo na kuamua kukaa chini kuwa haapo tayari kuondoka katika ofisi yao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...