![]() |
Ankal akiwa na Haji S.Manara Mkuu wa habari wa Simba leo jijini Dar es salaam |
Tumeanza kuandika hvyo hapo juu kwa maksudi kuonyesha sisi Simba tumeyakubali matokeo hayo ya dakika tisini za mchezo na tutumie nafasi hii kiungwana kabisa kuwapongeza watani wetu wa jadi kwa ushindi huo walioupata.
Pili tumshukuru Mungu kwa kutuwezesha kumaliza mchezo huo salama. Hapa Mungu ashukuriwe sana pamoja na wapenzi wetu pia. Sababu washabiki wetu wameonyesha utulivu wa kiunamichezo kwa kutokufanya fujo yoyote licha ya mwamuzi wa mchezo huo Israel Nkongo kuharibu mchezo kwa makusudi.
Refa Nkongo kwa dhamira ya kusudi jana aliamua kuwatoa wachezaji wetu mchezoni kwa kuanza kugawa kadi kwa wachezaji wetu pasi na sababu na tena kwa rafu zilezile kuacha wachezaji wa Yanga kucheza bila kuwaonya.
Kilichoshangaza washabiki wote waliokuwa uwanjani na walioangalia kwenye televisheni ni kumuacha mchezaji wa Yanga Donald Ngoma kuendelea na mchezo ilhali alimpiga kichwa cha maksudi mchezaji wetu Hassan kessi!!
Mbali ya vitendo hvyo wachezaji wetu wametulalamikia kutukanwa na mwamuzi wa mchezo huo Nkongo..
Tunaamini Tff watachunguza malalamiko yetu na kuchukua hatua stahiki kwa mwamuzi huyo ambaye kila mtu aliyeuona mchezo huo anakiri kuwa alishindwa kuumudu..
Mwisho na kwa umuhimu wa kipekee klabu ya Simba inaendelea kuwashukuru washabiki kwa utulivu wao licha ya vitendo vya mwamuzi huyo ambavyo vingeweza kabisa kuharibu amani iliyokuwepo uwanjani jana.
Tunawaomba waendelee kuwa watulivu katika kipindi hiki ambacho uongozi wenu umewaandikia TFF na bodi ya ligi ambazo tunaamini zitatenda haki..
Reclaming our glrory
Simba nguvu moja
Imetolewa na Haji S.Manara
Mkuu wa habari wa Simba
Simba sports club
27-9-2015
Nb.mchezo dhidi ya yanga ushapita na sasa tunajipanga kwa game ijayo.
Tunawaomba wapenzi wetu mjitokeze kwa wingi kwenye mechi yetu dhidi ya Stand united jtano ijayo ya tarehe 30-9-2015
👍👌👆☝☝Pamojaaaa. Sanaaa tuu!!
Ebwana nyie mnafanana hasa hizo pua , ongeeni na madingi wenu inaweza kuwa ni mtu na kaka yake
ReplyDeleteAcha kulialia wewe......kama kada na chama chao wao kila kitu nongwa ....ukivaaa gwanda tabu, mkikusanyika tabu, ukisema ukae ulinde chako tabu basi wapo wapo tu shiiiiiiiiiiiiiida.
ReplyDelete